SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

 • Serikali inatarajia kutumia Shilingi Tirioni 1.3 kupitia mkopo toka Exim benki
  ya nchini India kwa ajili ya miradi mikakati ya maji katika Miji 28 nchi nzima ili kukabiliana na tatizo la maji.
 • Hayo yamebaimnishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara  katika mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga-Uwasa) na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo.
 • Profesa Mkumbo alifanya ziara katika mamlaka hiyo kwa ajili ya kujionea utendaji wa kazi zao na zaidi kuona changamoto zinazowakabili watumishi hao na mamlaka husika na namna ya kuzitafutia ufumbuzi. Profesa Mkumbo alisema
  katika fedha hizo zaidi ya Shilingi Bilioni 140 zitainufaisha Miji ya Pangani,Muheza na Korogwe ambapo matarajio ya Serikali kuhakikisha
  kufikia malengo ya asilimia 85 Vijijini na 95 Mijini hadi kufikia 2025.
 • Alisema katika Miji hiyo Pangani imepangiwa kiasi cha Shilingi Bilioni
  22.5,Muheza Bilioni 5.6 na Korogwe kupitia mradi Mkuu wa maji Korogwe na
  Handeni BILIONI 112.5(HTM). “Matarajio ya Serikali ni kuhakikisha
  inapunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji vijijini na mijini na kufikia
  malengo yaliyojiwekea hadi kufikia mwaka huo wa 2025”Alisema Profesa
  Mkumbo.
 • Aidha lisema mchakato wa miradi hiyo mikakati umekwisha anza kwa hatua za awali ya usanifu na kupata Mtaalamu mshauri kwa ajili  ya miradi hiyo katika Miji ambayo imebainishwa kunufaika na fedha hizo kwa nchi nzima. Alisema hadi kufikia juni mwaka huu miradi hiyo itakuwa imekwisha dizainiwa na mwezi Sept wakandarasi watatkiwa kuwa katika maeneo ya kazi katika miji hiyo 28 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
 • Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka makandarasi kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na watambue Serikali haitomzulumu mkandarasi
  yoyote na fedha zao zitalipwa bila ya mashaka yoyote. “Tunajua madai ya
  makandarasi wengi nchi nzima lakini tutawalipa waondoe shaka koila
  mwezi tulipa shilingi Bilioni 8-12 hivyo tutwalipa tu”Alisema.
 • Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na
  Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
  alisema changamoto kubwa kwa sasa mkoani hapa ni namna ya kuongeza
  huduma ya taka ndani ya Jiji.“Mbali na fedha zilizoainishwa na
  Katibu Mkuu lakini tunatarajia kupokea zaidi ya shilingi bilioni 400 kwa
  ajili ya miradi ya maji taka,kubadilisha miundombinu ya mabomba,ujenzi
  wa matank”Alisema Mhandisi Hilly.
 • Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kulia akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAKAZI WA KIGWA KUPATA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA GHARAMA YA BILIONI 10

Serikali imeamua kupeleka maji katika Kata ya Kigwa wilayani Uyui kupitia mradi wa ujenzi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *