MIRADI YA MAJI 547 INATEKELEZWA KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI – PROF MBARAWA

  • Jumla ya miradi ya maji 547 inaendelea kutekelzwa nchini yenye thamani ya shilingi trilion 3.76, miradi hiyo ambayo imegawanyika katika makundi mawili ambapo ipo miradi inayotekelezwa mjini na mingine vijijini.
  • Hayo yamesema na Waziri wa Maji na Umwangiliaji Prof. Makame Mbarawa wakati akizungumza kuhusu miaka minne ya serikali madarakani ambapo amesema katika jijini la Dar Es Salaam kuma miradi tisa ya maji inaendelea ambayo  ina gharama ya shilingi bilioni 232 kati ya miradi hiyo ipo miradi mitatu ambayo inapata pesa moja kwa moja kutoka Serikalini na miradi sita inafanywa na mamlaka ya maji  Dar Es Salaam.
  • Akitaja miradi hiyo Waziri Mbarawa amesema mradi wa kwanza ni wa usambazaji maji kutoka katika matanki ya maji Chuo Kikuu Dar Es Salaam mpaka Bagamoyo ambao gharama yake ni shilingi bilioni 77 na upo katika hatua za mwanzo ambapo utahusisha ujenzi wa matanki matatu na kila tanki moja litakuwa na uwezo wa mita za ujazo millioni sita.
  • Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na vituo viwili vikubwa vya kusukumia maji kupeleka katika maeneo mbalimbali na utaweza kujenga kilomita 1,461 katika maeneo ya jiji la Dar Es Salaam na Bagamoyo ambapo baada ya kukamilika kwa kazi mradi huo utaweza kuunganisha wateja 64,000 ambao watapata huduma ya maji.
  • Akizunguimzia mradi wa pili katika jiji Dar Es Salaam amesema kuwa mradi wa usambazaji maji kutoka Ruvu juu kupeleka Dar Es Salaam ambapo mradi huo umejenga mtanki matano ambapo kila tanki linauwezo wa kuifadhi maji lita milioni 6 pia amesema mradi huo umejenga tanki moja lenye uwezo wa kuifadhi maji lita milioni 5, aidha amesema mradi huo umejenga kilomita  317 za usambazji maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam.
  • Waziri Mbarawa amesmea mradi huo umejenga vituo vinne vya kusambazia maji  katika maeneo mbalimbali ikiwemo Goba na Wazo, na mradio huo umekamilika kwa asilimia 98, ameogeza kuwa mradi mwingine ni wa Kigamboni unao gharimu shilingi bilioni 29 ambapo visima 20 vimechimwabwa katika maeneo tofauti  Kimbiji visima 12 na visima 8 Mpera.
  • ”kazi inayofata sasa hizi ni kusambaza maji hayo ambapo tuna mradi mwingine shilingi bilioni 12.45 ambao sasa mradi huo kazi ya kubwa ni kuendeleza visima vitano pamoja na ujenzi wa tanki lenye ujazo lita milioni 15 pamoja na usambazji maji hayo kwa wateja ambao utakuwa na kilometa 85 za usambazaji  kazi hiyo imeanza na  tayari tumempata mkandarasi tunaamini itapofika mwakani kabla ya juni utakuwa umekamilika” amesema Waziri Mbarawa
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT HASSAN ABBASI AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.