SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

 • Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imezipa Kandarasi ya thamani ya shilingi 2.9 bilioni kampuni tatu za vijana wa Kitanzania ili kutekeleza mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House).
 • VIJANA-10Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akizindua mafunzo hayo Januari 05, 2019 yanayoendelea katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro.
 • Programu hiyo ambayo itatumia jumla ya shilingi 2.9bilioni katika utekelezaji wake ambapo kampuni zilizoshinda kandarasi hiyo ni Kampuni za vijana wazalendo wa kitanzania ambao ni wabobezi katika masuala ya kilimo ikiwemo kampuni na Royal Agriculture Ltd, Holly Green Agriculture Group Ltd, na SUGECO.

VIJANA-1

 • Mafunzo haya yatafanyika katika Mikoa yote Tanzania Bara na kuhakikisha Halmashauri 84 zinafikiwa kwa awamu hii ya kwanza lengo likiwa ni kuwajengea vijana ujuzi kupitia kilimo cha kisasa ambapo tayari kwa mwaka huu wa fedha imeanza mafunzo hayo kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba (greenhouse).
 • “Kwa kuanzia tutahakikisha kila Halmashauri tunatoa mafunzo kwa vijana 100 na kati yao vijana 20 watapatiwa mafunzo ya kujenga Vitalu Nyumba ili kwa wale watakaopenda kuendelea na kilimo hiki wasikose wataalamu wa kuwajengea Vitalu hivyo ”Alisisitiza Mavunde.

VIJANA-2

 • Aidha, Amewataka vijana kutumia fursa ya kilimo katika kujikwamua na changamoto za ajira na kuelezea umuhimu wa kilimo katika kuongeza pato la Taifa na kuchangia katika uchumi wa viwanda nchini.
 • “Wote tunatambua kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu kwani kwasasa kimeajiri takribani asilimia 65.7 ya nguvu kazi nchini na kinachangia asilimia 29.1 ya pato la taifa, pia sekta ya kilimo ndiyo chanzo kikuu cha chakula, ajira, na malighafi ya viwanda”Alisisitiza Mavunde.

VIJANA-3

 • Naye Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya wenye ulemavu Mh Ikupa Stella Alex amebainisha kwamba program hii na jumuishi na hivyo kutoa rai kwa watekelezaji wa program hii katika ngazi za mikoa kuhakikisha wanawajumisha pia watu wenye ulemavu ili kunufaika na program hii.VIJANA-4
 • Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario alieleza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanafikia kundi kubwa la vijana nchini na kushukuru mchango wa serikali katika programu za ukujazi ujuzi kwa vijana.
 • VIJANA-5
 • “Kipekee naishukuru Wizara hii kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha inatoa mchango mkubwa kwa vijana na kusaidia kuwakwamua kiuchumi.”Alisema KimarioVIJANA-7VIJANA-8
 • “Tunataka vijana wawe mstari wa mbele katika kilimo cha kisasa ili kuendana na mazingira ya sasa na kujikwamua katika kundi la wasio na ajira nchini”.Alisistiza Msaki.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI SHONZA: WAZAZI NDIYO WALEZI WA KWANZA WA MTOTO

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wazazi na familia kuwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *