WAZIRI MKUU AFUNGUA JENGO LA TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

  • Asema kukamilika kwa taasisi hiyo kutakuwa na manufaa makubwa kwa jamii
  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua Jengo la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), wilaya ya Magharibi ‘B’ lililojengwa kwa ghararama ya sh. bilioni 4.2.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa kitengo cha kompyuta Safaa Haroub, baada ya kuweka jiwe la msingi wa jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” – Unguja
  • Afungua jengo hilo (Jumanne, Januari 8, 2019) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12, 1964.Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa Jengo la taasisi hiyo kuna manufaa makubwa kwa jamii ikiwemo kutoa elimu ya ufundi itakayowasaidia vijana kujiajiri na kuondokana na utegemezi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi wa jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” – Unguja
  • “Kusaidia azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 na msukumo katika sekta ya viwanda kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa katika sehemu mbalimbali pamoja na Serikalini.”Amesema manufaa mengine ya KIST ni kutoa mafunzo ya fani mbalimbali zinazokwenda sambamba na mabadiliko ya ulimwengu katika Nyanja za sayansi, teknolojia na ualimu.
  • Kadhalika, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa KIST ubuni mbinu mbalimbali na utafute miradi mingine ya ujenzi itakayosaidia kuwa na miundombinu ya kisasa ya kutolea elimu.Amesema uongozi wa taasisi hiyo hauna budi kuweka mikakati ya kushirikiana na taasisi nyingine zinazotoa mafunzo ya ufundi ndani na nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kitabu kwenye maktaba ya jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” – Unguja baada ya kufungua jengo hilo
  • Waziri Mkuu amesema kulingana na maendeleo ya kiteknolojia na mahitaji ya soko uongozi wa KIST ujipange kutoa mafunzi ya biomedical Engineering na kuimarisha mafunzo ya matengenezo ya ndege na urubani katika ngazi ya stashahada.
  • Awali, Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema Wizara yake itaendeleza taasisi hiyo ili kuwaendeleza vijana na baadae waweze kujiajiri na kuajiri.Alisema vijana wanaohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika taasisi hiyo wanapewa mikopo ya masharti nafuu na Serikali baada ya kujiunga kwenye vikundi.
  • Waziri Huyo, alisema wahitimu hao kabla ya kupewa mikopo wanaandika andiko la miradi ambayo watakwenda kuitekeleza ambapo tayari vikundi zaidi ya 10 vya vijana vimeshawezeshwa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU AMPONGEZA BONDIA SALIM MTANGO ALIYESHINDA MKANDA WA DUNIA WA UBO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *