SERIKALI HAINA MPANGO WA KUONGEZA MIKOA MIPYA – RAIS MAGUFULI

  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo ya utawala ikiwemo kuanzisha mikoa mipya na badala yake imejipanga kuimarisha huduma na mahitaji ya miundombinu iliyopo ili kuwaletea maendeleo wananchi.
  • Amezungumza hayo Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru yenye urefu wa kilometa 193, Rais Magufuli amesema hayo akiwajibu wananchi waliotaka kuanzishwa kwa mkoa mpya huko Tunduru mkoani Ruvuma
  • “Serikali inakusudia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, maji, elimu n.k katika maeneo waliopo”alisisitiza Rais Magufuli
  • Ameongeza kuwa katika awamu yake ya Uongozi, suala la kuongeza maeneo ya utawala halipo na badala yake kuwataka Viongozi wa maeneo hayo wajipange katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya fedha zilizopo kwenda katika kujenga ofisi mpya za Wakuu wa Mikoa mipya na kuwalipa mishahara viongozi hao.

Nukuu za Rais 05/04/2019 Tunduru,Ruvuma

  • “Siwezi ni kazi yao Tsh Mil 200 kwa kujenga ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tunduru! kwahiyo Waziri wa Tamisemi una deni hapa la kuwaongezea Tsh mil 200 hospitali ile waipanue! Tuwe na wodi za kutosha kwaajili ya kina mama na watoto!! Teletext vifaa vya kutosha”
  • “Kwa sababu mahitaji ya wananchi wa Tunduru, si kumuona Mkuu wa Mkoa na kitambi chake akitembea barabarani; Wanataka shida zao wanatunduru zimaliziwe! Unaweza ukagawanya Tunduru hata ukawa na mikoa mitatu humu. Hata ukasema sasa kila tarafa iwe mikoa”
  • “Kwa hiyo kitu kikubwa katika maendeleo kinachohitajika si kuwa na mkoa ni kupeleka vitu vinavyohitajika ktk eneo lile. Ukiufanya mkoa wa Tunduru ukaacha kuwapelekea umeme, hujawasaidia Tunduru”
  • “Mmeimba wimbo pale mnataka sasa hapa pawe mkoa! Ni mawazo mazuri..Lakini inawezekana wakati haujafika! Wilaya hii kwenye sensa ya mwaka 2012 ilikuwa na watu laki 3 na kwa idadi hii ya kuongezeka inawezekana sasa wameshafikia laki 5”

    Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *