WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA JUMUIA YA MABOHORA

  • Jumuia ya Mabohora Nchini imesema imeanza jitihada za kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli za kuhamia Dodoma kwa kuanza kuhamishia baadhi ya biashara zao mkoni humo.
  • Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Mabohora Zainuddin Adamjee akiwa na ujumbe wake walipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki profesa Palamagamba John Kabudi katika Ofisi ndogo za wizara hiyo jijini Dar es salaam.
  • Amepongeza pia jitihada zinazofanywa na Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa muongozo wa Rais Dkt John Pombe Magufuli wa kuwataka mabalozi wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi kuegemea katika diplomasia ya Uchumi kwa kuhamasisha wawekezaji kuja hapa nchini kwani jambo hilo litaiwezesha Tanzania kupiga hatua za haraka za kimaendeleo na kufikia azma ya serikali ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo 2025 na kwamba jumuia hiyo kwa sasa imeanza kuwekeza katika ujenzi wa hospitali kubwa na ya kisasa inayojengwa jijini Dar es salaam na kwamba itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuwahudumia wagonjwa mabalimbali hasa wa maradhi ambayo wagonjwa wake hulazimika kusafirishwa nje ya nchi.
  • Kwa upande wake waziri wa Mambo ya ndani na Ushirikiano wa Afrika Mashariki profesa Palamagamba John Kabudi ameushukuru ujumbe huo kwa kumtembelea ofisini kwake na kuitaka kuendelea kuwahamsisha wanajumuia wenzao wa mabohora duniani pamoja na wafanyabiashara wengine kuja kuwekeza hapa nchini kwa kuwa mazingira ya uwekezaji yameboreshwa zaidi.
  • Aidha amewapongeza mabohora wote nchini kwa uzalendo wao kwa Taifa la Tanzania na kuwataka kuendelea kudumisha Amani,umoja na Mshikamano miongoni mwao ili kuliwezesha Taifa kuendelea kuwa kisiwa cha Amani.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI ZUNGU AHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA MALIASILI WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

             

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *