RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 30 KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI KUTUMIA HUDUMA ZA KAMPUNI YA TTCL

  • Rais Dkt.John Magufuli siku 30 Ofisi ya Rais-IKULU, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma,kutum kutumia huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Nchini (TTCL)ikiwemo laini, ili kupanua huduma za mawasiliano ya Mtandao wa Kampuni hiyo nchini.
  • Akizungumza wakati wa Hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali la Tsh Bilioni 2.1 kutoka TTCL, Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa TTCL kumuorodheshea nam,ba za simu za Viongozi na Watendaji wote wa Serikali ikiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu kuona kama wanatumia laini za simu za TTCL.
TT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Waziri Kindamba wakati akiwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Shirika hilo katika Gorofa la Extelecom Posta jijini Dar es Salaam.
  • Aliongeza kuwa tangu atoe agizo lake mwaka jana, kuhusu matumizi ya huduma za mawasiliano ya TTCL katika Ofisi mbalimbali za Umma, hakuna Ofisi yoyote ilitekeleza agizo hilo ukiondoa baadhi ya Taasisi chache ikiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania na Jeshi la Polisi Nchini.
  • “Nimefurahi alipokuwa akitaja Taasisi na Mashirika ambayo yamejiunga moja kwa moja na kutumia huduma za TTCL, nilisikitika sana niliposikia Ofisi yangu haikutajwa, pia Ofisi ya Chama changu cha mapinduzi, sasa kama wamesikia na wako hapa nataka kipindi cha mwezi mmoja tuanze kutumia simu za TTCL”, Rais Magufuli.

TT

  • Aidha Rais Magufuli alizitaka Ofisi zingine za Serikali kutumia huduma za Kampuni ya Mawasiliano Nchini ili kuinua na kuimarisha utendaji kazi wake katika nyanja mbalimbali za maendeleo nchini na kuzitaka Taasisi zingine ziige huo kwa vitendo na siyo maneno.
  • “Si Ofisi ya Makamu wa Rais, Si Ofisi ya Waziri Mkuu, Si Ofisi ya Rais, Si Wizara ya Fedha, hata Wizara yako ya Mawasiliano na Uchukuzi nayo haijatajwa hapa, nataka kusema tusipounga Mkono, vyetu tutachezewa mno, tusipowaimarisha hawa TTCL, hawatafika mbali, lakini wakipata ushirikiano matokeo tutayaona”, Rais Magufuli.

TT

  • Rais Magufuli alieleza kuwa kabla ya Shirika hilo halijarudishwa Serikalini, katika kipindi cha miaka 15 kutoka mwaka 2001 TTCL ilikuwa ikipata hasara ya Tsh Bilioni 15 kila mwaka, huku likishindwa kutoa gawio lolote kwa Serikali.
  • “Wakati Shirika hili likiendeshwa na Wabia wetu, lilikuwa halitoi gawio lolote, lakini pia lilikuwa likipata hasara ya Bilioni 15 kwa mwaka, kwa hiyo mnaweza mkaelewa hii ina maana gani kwenye uchumi wa nchi, hivyo basi kuweza kufikia hatua hii ya kupata faida ya Tsh.bilioni 8.3, na kuweza kutoa gawio la Serikali Tsh.bilioni 2.2 ni mafanikio makubwa’ alisema Rais Dkt Magufuli.

TT

  • Pia Rais Magufuli alisema kuwa Sekta ya Mawasiliano kwa sasa imepanuka  nchini na kuwezesha sekta nyingine kufanya kazi kwa ufanisi kwani katika sekta mbalimbali kwa sasa sekta hii inahitajika sana.
  • “Sekta ya Mawasiliano imesaidia kukua kwa sekta nyingine kama sekta ya fedha, ambapo mwaka jana miamala ya fedha ilifanyika kwa njia ya kimtandao ilikuwa na thamani ya Tsh Trilioni 139.2 sawa na Trilioni 11.6 kwa mwezi, lakini pia sekta ya mawasiliani ni kichocheo kikubwa kwa Sekta za Elimu, Afya, Biashara, Kilimo, Viwanda  Ufugaji, Utalii na Ujenzi”, Rais Magufuli.
TT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vitendea kazi mbalimbali katika makumbusho iliyopo ndani ya Ofisi za Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL jijini Dar es Salaam.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *