JWTZ KUHAKIKI UPYA VIJANA WALIOKIUKA USAJILI WA KUJIUNGA NA JKT

  • Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeamua kufanya upya uhakiki wa kina utaratibu wa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa vijana wanaojiunga kwa kujitolea baada ya kubaini baadhi yao kufanya udanganyifu wakati wa usaili unaoendelea sasa.
  • Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Jeshi Luteni Kanali Gaudence Ilonda amebainisha kwamba katika uandikishaji wa vijana kwa nafasi zilizotolewa mwaka huu, kuna wimbi la vijana kuhama kutoka mikoa mbalimbali kwenda mikoa mingine kwenda kutafuta nafasi kinyume na taratibu za Jeshi.
    Pia amesema Jeshi limebaini wapo baadhi ya vijana katika zoezi la kujiandikisha linaloendelea sasa wamegushi nyaraka mbali mbali ikiwemo vyeti vya kuzaliwa, elimu na kadhalika kinyume na taratibu za kujiunga.
  • Halikadhalika Jeshi limegundua ikiwemo wa vikundi vya utapeli vinavyolaghai vijana na walezi wao watoe pesa ili wapewe nafasi ya kujiunga na Jeshi. Jeshi limejipanga kukomesha matapeli wote wanaofanya vitendo hivyo katika uandikishaji wa sasa.
  • Luteni Kanali Ilonda amesema Jeshi pia limekuwa likipokea maombi ya viongozi mbali mbali wanaoomba nafasi za kujiunga katika usaili wa mwaka huu. Ameeleza kwamba baadhi ya viongozi wamediriki hata kupeleka majina ya vijana Makao Makuu ya Jeshi na ameonya viongozi hao haijulikani wana nia gani kuwaombea vijana kwa idadi kubwa na Jeshi halitakaa kimya na litachukua hatua juu ya viongozi wote waliowasilisha majina ya vijana wapewe nafasi Jeshini.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

TUNAJUA WATENDAJI WAKIPATA MAKAZI BORA WATAONGEZA UFANISI KATIKA KAZI

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amempongeza Rais Dkt John …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *