Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Sadik (kushoto) akiongoza Kikao cha Kamati jijini Dodoma kilichopokea taarifa za Ofisi ya Makamu wa Rais.
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) leo Agosti 27, 2019 imewasilisha taarifa zake mbili kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira jijini Dodoma.
Taarifa zilizowasilishwa ni ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yanayohusiana na majukumu ya Wizara yaliyotokana na Mapendekezo ya Kamati hiyo katika taarifa yake ya mwaka iliyowasilushwa katika Mkutano wa Bunge wa Februari 2019.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Suleiman Sadik pia imepokea taarifa ya Mazingira kwa ajili ya kujijengea uelewa kuhusu Tathmini ya Athari ya Mazingira (TMA).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. George Simbachawene akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. Mussa Sima akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kilichofanyika jijini Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Sadik (kushoto) akiongoza Kikao cha Kamati jijini Dodoma kilichopokea taarifa za Ofisi ya Makamu wa Rais.Kuanzia kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. George Simbachawene, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. Mussa Sima, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa William Mwegoha na Mkurugenzi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka wakifuatilia kikao hicho.