WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 1683 KUHUDHURIA KONGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI DAR

B 2-01
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) jijini Dar es salaam leo kuhusu kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda linalotarajiwa kufunguliwa kesho na Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ukumbi wa Julius Nyerere.
  • Wafanyabiashara zaidi ya  1683 wanatarajiwa kihudhuria  katika kongamano la kibiashara la nchi ya nchi mbili, Tanzania na Uganda litakalofanyka katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  • Mkutano huo wa wafanyabiashara zaidi ya 1056 wa Tanzania na wauganda 426  utafunguliwa kesho Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli wakishirikiana na Rais  wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
  • Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Waziri wa biashara na Viwanda Innoncent Bashungwa amesema kuwa maandalizi ya kufanyika kongamano la biashara kati ya  nchi hizi mbili Tanzania na Uganda yamekamilika na hivi sasa tunapokea wafanyabiashara kutoka nchini uganda kwaajili ya kesho mapema saa tatu asubuhi kongamano hilo lifunguliwe na marais wetu wa Tanzania na Uganda.
  • Hata hivyo  Waziri Bashungwa amesema kuwa wafanyabiashara hapa mchini wajiandae  vyema katika kubadilishana uzoefu wa masuala ya biashara na wafanyabiashara wa  Uganda ili kuunganisha dunia pamoja.
  • Amesema kuwa wafanyabiashara wa hapa nchini pamoja na taasisi mbalimbali za serikali watahudhulia mkutano huo ili kujadili sera na vikwazo vya kiuchumi na kibiashara katika nchi hizo mbili ili waweze kutatua na kufanya biashara bila vikwazo vigumu vya kibiashara
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

Oni moja

  1. The Writing has become a go-to resource for me. The effort you put into The posts is truly appreciated.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *