TANZANIA KUNUFAIKA NA MIKOPO YA KUENDELEZA MIRADI YA MIUNDOMBINU KUTOKA BENKI YA ‘ASIAN INFRASTRUCTURE INVESTMENT’.

11-01
Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) kulia, na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Mohammed Abdiwawa. Kulia kwa Mhe. Mpango ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Mashimba Ndaki na kushoto kwa Mhe.Abdiwawa ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga.
  • Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.
  • Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika kutoka katika Benki hiyo.Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC
22-01
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) akiwa katika mazungumzo na Bw. Danny Alexander Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ yaliyofayika katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC. Kushoto kwa Mhe.Waziri ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana, Dkt.Yamungu Kayandabila.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TRA – WAFANYABIASHARA MSIJIHUSISHE NA BIASHARA ZA MAGENDO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara na wachuuzi wanaoishi jirani na fukwe za Bahari …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *