RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA AALCO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA

  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli  amekutana na viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali.
j-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akigana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa (Wakwanza kulia) na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang (wakwanza kushoto) mara baada ya Mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
  • Viongozi wa AALCO waliokutana na Mhe. Rais Magufuli ni Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO watatu ambao ni Bw. Yukihiro Takeya (Japan), Bi. Wang Liyu (China) na Dr. Ali Garshasbi (Iran).
d-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Amon Mpanju Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania) mara baada ya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
  • Mhe. Rais Magufuli amewashukuru na kuwakaribisha wajumbe wa AALCO nchini Tanzania na amewahakikishia kuwa Serikali inatambua kazi inayofanywa na taasisi hiyo tangu ijiunge nayo mwaka 1965 na kuwa mwanachama kamili kuanzia mwaka 1973.
  • Mhe. Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa AALCO kutekeleza malengo ya taasisi hiyo kama alivyoelezwa na viongozi hao, na ametoa wito wa kuendelea kuzitetea nchi wanachama hasa zinazowekewa vikwazo mbalimbali.
g-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou, ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
  • Ametolea mfano wa Zimbabwe ambayo imewekewa vikwazo kwa miaka mingi hali inayosababisha wananchi wa Zimbabwe kuteseka.
  • Rais wa AALCO Mhe. Balozi Mahiga na Katibu Mkuu Mhe. Prof. Kennedy Gastorn wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kupata fursa ya kukutana nae na wameahidi kuwa AALCO itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya Asia na Afrika.
f-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Bi. Wang Liyu Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria wa China mara baada ya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
  • Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba Mhe. Amon Mpanju.
  • Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
e-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina) mara baada ya mazungumzo na Viongozi hao wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
  • Rais Magufuli amemshukuru Ndg. Yezhou kwa kutembelea hapa nchini kwa mara ya pili na pia ameishukuru China kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano mzuri na Tanzania ikiwemo mchango mkubwa wa chama cha CPC ambacho kinajenga Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uongozi kwa nchi 6 zenye vyama vya ukombozi vilivyoshirikiana na CPC ambazo ni {Tanzania (CCM), Afrika Kusini (ANC), Zimbabwe (ZANU-PF), Msumbiji (FRELIMO), Angola (MPLA) na Namibia (SWAPO)}.
h-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang pamoja na Kanali Ngamela Lubinga Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa Kimatifa wa Ccm ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
  • Rais Magufuli pia amemuomba Ndg. Yezhou kufikisha shukrani zake kwa Rais wa China na Mwenyekiti wa CPC Mhe. Xi Jinping kwa kutoa tuzo kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuiwezesha China kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
a-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019.
  • Rais Magufuli amemhakikishia kuwa Sera za Tanzania kuhusu China hazijabadilika na amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika jitihada mbalimbali za maendeleo.
i-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang na Kanali Ngamela Lubinga Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa Kimatifa wa Ccm mara baada ya mazungumzo yao ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
  • Mazungumzo hayo yamehudhriwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke.
b-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO watatu ambao ni Bw. Yukihiro Takeya (Japan), Bi. Wang Liyu (China) na Dr. Ali Garshasbi (Iran) pamoja na Amon Mpanju Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania), ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NJE DKT. NDUMBARO AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI TANO HAPA NCHINI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *