WAZIRI MKUU MAJALIWA KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI NCHINI AZERBAIJAN

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwwa ameutaka ubalozi wa Tanzania nchini Urusi uratibu mipango ya wafanyabiashara wa Urusi wanaokusudia kuja nchini kuwekeza kwa kuwaunganisha na Taasisi na Wizara husika ili waweze kuwekeza mitaji yao kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.
  • Ametoa agizo hilo jana (Alhamisi, Oktoba 24, 2019) baada ya kugundua uwepo wa
    wafanyabiashara wengi wa Urusi wanakusudia kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji pamoja na kutafuta wafanyabiashara wa Kitanzania watakaoungana nao katika uwekezaji wanaokusudia kuufanya.
  • “Tayari miadi imekwishawekwa ya kuwakaribiasha wawekezaji wa Urusi kuja Tanzania kwa ushawishi wa kwangu mwenyewe pamoja na ushawishi wa wafanyabiashara wa Tanzania, hivyo nisingependa wafanyabiashara hao wasumbuliwe au kukatishwa tamaa katika kutimiza nia yao hiyo.” Waziri Mkuu alisisitiza.
  • Alisema Mkutano baina ya Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na
    Urusi uliomalizika jana Oktoba 24, 2019 ulilenga kujenga uhusiano mzuri zaidi katika nyanja mbalimbali hususani za kiuchumi.
  • Akizungumza baada kumalizika mkutano huo kwenye ukumbi wa Olympic Park wa Sochi nchini Urusi, Waziri Mkuu alisema Urusi imeutumia mkutano huo kueleza bayana maeneo ambayo wako tayari kushirikiana na Afrika katika kuwekeza kwa faida ya pande zote mbili.
  • Waziri Mkuu aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na uuzaji wa zana za kilimo kama vile matrekta, sekta ya mafuta na gesi pamoja na madini, Ujenzi wa miundombinu hasa reli, masuala ya elimu hasa utoaji wa nafasi za mafunzo nchini humo.
  • Alisema kwa upande wake Tanzania imejinadi vizuri ikIngozwa na yeye mwenyewe kwani alifanya mazungumzo na viongozi wa makampuni zaidi ya manane ya Urusi ili kuyashawishi yawekeze nchini na yote yalikubali kufika Tanzania mapema iwezekanavyo.
  • “Viongozi wa makapuni yote niliyopata nafasi ya kuzungumza nao wamesema wako tayari kuja nchini ili waweze kufanya mazungumzo na Serikali pamoja na wafanyabiashara wazalendo ambao wako tayari kuungana na wafanyabiashara hao katika kuwekeza nchini Tanzania.”
  • Waziri Mkuu alisema viongozi hao walimueleza maeneo ambayo wao wanaamini kuwa
    wanafanya vizuri na wangependa kupata kibali cha kuwekeza Tanzania baada ya mazungumzo yao na Serikali. Pia walieleza ni kwa namna gani Taifa litanufaika na uwekezaji wao.
  • Alisema, tayari wafanyabiashara binafsi 18 wa Tanzania walijitokeza kushiriki katika Mkutano huo na walifanya kazi kubwa na nzuri ya kuwahabarisha wenzao wa Urusi kuhusu mazingira mazuri ya kuwekeza yaliyopo nchini hasa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuondoa kero, kanuni na taratibu ziliokuwa zikiyafanya mazingira ya uwekezaji kuwa magumu.
  • Awali, akizungumza kwenye Mkutano baina ya Wakuu wa nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi, Waziri Mkuu alisema kwa sasa Tanzania ni nchi sahihi kwa uwekezaji kwa wanaotaka kuwekeza barani Afrika kwani imedhamiria kukuza uchumi wake na kufikia wa kati ifikapo 2025 kwa kupitia sekta ya viwanda. Pia ni nchi yenye amani na utulivu.
  • “Nchi yetu imejaliwa kuwa na maliasili nyingi ambazo vilele ni malighafi kwa viwanda kama vile mazao ya kilimo, misitu, bahari, maziwa, madini na mbuga za wanyama ambazo ni kivutio cha watalii,” alifafanua Waziri Mkuu.
  • Leo Oktoba 25, 2019 Mheshimiwa Majaliwa ataondoka nchini Urusi kwenda nchi ya Azerbaijan ambako pia atamwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote. Mkutano huo ni wa siku mbili.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, OKTOBA 25, 2019.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

7 Maoni

  1. Ruben Diogo da Silva Neves https://ruben-neves.prostoprosport-ar.com is a Portuguese footballer who plays as a midfielder for the Saudi Arabian club Al-Hilal and the Portuguese national team. Currently, Ruben Neves plays for the Al-Hilal club wearing number 8. His contract with the Saudi club is valid until the end of June 2026.

  2. Mohammed Khalil Ibrahim Al-Owais https://mohammed-alowais.prostoprosport-ar.com is a Saudi professional footballer who plays as a goalkeeper for the national team Saudi Arabia and Al-Hilal. He is known for his quick reflexes and alertness at the gate.

  3. Larry Joe Bird https://larry-bird.prostoprosport-br.com American basketball player who spent his entire professional career in the NBA ” Boston Celtics.” Olympic champion (1992), champion of the 1977 Universiade, 3-time NBA champion (1981, 1984, 1986), three times recognized as MVP of the season in the NBA (1984, 1985, 1986), 10 times included in the symbolic teams of the season (1980-88 – first team, 1990 – second team).

  4. Karim Benzema https://karim-benzema.prostoprosport-cz.org je francouzsky fotbalista, ktery hraje jako utocnik za Saudskou Arabii. Arabsky klub Al-Ittihad. Hral za francouzsky narodni tym, za ktery odehral 97 zapasu a vstrelil 37 branek. V 17 letech se stal jednim z nejlepsich hracu rezervy, nastrilel tri desitky golu za sezonu.

  5. Virgil van Dijk https://virgil-van-dijk.prostoprosport-cz.org Nizozemsky fotbalista, stredni obrance, kapitan anglickeho klubu Liverpool a kapitan nizozemskeho narodniho tymu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *