WAZIRI LUKUVI AWATAKA WAFUGAJI KUWEKA UZIO ILI KUEPUSHA MIGOGORO NA WAKULIMA

  • Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza wafugaji wote wanaomiliki maeneo yenye hati kuweka uzio katika maeneo yao ili kuepuka mifugo yao kwenda maeneo ya wakulima na kusisitiza kufanyika ufugaji wa kisasa.
  • Lukuvi alitoa agizo hilo wilayani Kilosa mkoani Morogoro wakati akizungumza na uongozi wa wilaya ya Kilosa na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara ya kutatua migogoro ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.
  • Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na uongozi wa wilaya ya Kilosa pamoja na Watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wakati wa muendelezo wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani Morogoro.
  • Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ameomba kufanyika ukaguzi wa ardhi za vijiji kwa kuwa baadhi yake watu wamejimilikisha, wameuza na mengine kufanyika mgawanyo usio sahihi.
  • Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema vijijji viwili vilivyosajiliwa katika maeneo ya hifadhi wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro vitaendelea kubaki katika maeneo hayo kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia vijiji 920 vilivyokuwa katika maeneo ya hifadhi kuendelea kubaki maeneo hayo.
  • Lukuvi amevitaja vijiji vya Mjambaa kilichoko katika shamba la Mbugani Estates lenye ukubwa wa ekari 1600 na kile cha Mambegwa kuwa vitaendelea kutambuliwa na kuagiza  halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwenda kuvipima na kuanisha shughuli za kilimo na makazi katika vijiji hivyo
Ad

Unaweza kuangalia pia

SEKTA YA ARDHI YATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO NCHINI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya amezitaka idara mbalimbali za Serikali kuipa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *