MUHIMBILI IMEPIGA HATUA KUBWA UTOAJI WA HUDUMA ZA KISASA KWA GHARAMA NAFUU

 • Serikali imeendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya ambayo imepewa kipaumbele ili kuwawezesha wananchi kupata huduma zilizobora kama vile upatikanaji wa dawa, vipimo ambavyo vilikuwa vinapatikana nje ya nchi.
 • Katika miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Hospitali ya Taifa Muhimbili imepiga hatu kubwa katika kutekeleza ya maagizo ya Mhe. Rais kwa kuweka miundombinu safia na kuwapatia wananchi huduma zilizobora.
 • Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili, Prof. Lawrence Museru ameeleza, “baada ya Serikali ya Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kuingia madarakani alitoa maagizo mbalimbali, ikiwemo la kuwapatia vitanda wagonjwa waliokuwa wanalala chini, kutengeneza mashine za CT-Scan na MRI, ambapo kero hizo zilitatuliwa na mpaka sasa mashine hizo zinafanya kazi” amesema Prof Museru.
1-01
CT SCAN
 • Hospitali ya Taifa Muhimbili katika miaka Minne ya utendajio wa Rais Magufuli imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa upatikanaji wa dawa ambapo kwa sasa wagonjwa wanapata dawa zaidi ya asilimia 96,  ukilinganisha na wastani wa asilimia 40 hapo awali, akasema, “Serikali inatoa shilingi Bil 1.5 kununua dawa kila mwezi sawa na bilioni 18 kwa mwaka”.
 • “Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza maagizo ya Rais, na hasa lile la kupeleka wagonjwa nje kwani mpaka sasa hospitali imeweza kupeleka wataalam wabobezi masomoni kwenye mafunzo mbalimbali yatakayogharimu Tsh.bilioni 3.597”, Prof. Museru
 • Akaongeza kuwa wahusika ni wataalamu  wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini, maabara, madaktari bingwa, radiolojia, saratani za damu, na hatua hiyo imepunguza kupeleka wagonjwa nchi za nchi.
2-01
DIGITAL XRAY
 • Kadhalika, Hospitali imefanikiwa Vifaa vya  upandikizaji vya kusaidia watoto kusikia ambapo mpaka sasa wagonjwa 34 wamenufaika, wawili kati yao wamelipia matibabu hayo, huku 32 wakigharamiwa na serikali ambayo ilitoa kiasi cha shilingi Bil.1.15, sawa na shilingi milioni 36 kila mmoja, hivyo kuokoa bil. 2.05 kama wangetibiwa nje ya nchi.
 • Prof.Mseru alisema kuwa juhudi kubwa zilizowekwa na serikali ya awamu ya nne mojawapo ni upandikizaji figo , ambapo mpaka sasa wagonjwa 51 wameweza kutibiwa kwa ghrama ya Tsh.Bil.1.530 kwa mgonjwa mmoja, na kuokoa Tsh.Bil.4.590, wakati hapo awali miaka 15 iliyopita, Serikali ilishasafirisha wagonjwa 150 nje ya nchi.
3-01
MRI
 • Eneo lingine, Hospitali imeweza kupiga hatua kubwa kwa kuimarisha vifaa tiba vya kisasa, ikiwemo CT-Scan, Digital X-Ray, MRI, X-Ray ambavyo vimesaidia katika kutoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa, ambao kiasi kikubwa walikuwa wakisafirishwa kwenda nje ya nchi na kutumia gharama kubwa.
 • “Novemba 2017, Hospitatli ya Muhimbili ilifanikiwa kuanzisha huduma za tiba ya Radiolojia, ikishirikiana na wataalam kutoka Kenya na kutoka Chuo kikuu cha Yale  kilichopo Marekani,  ambapo mpaka sasa tumeweza kuwahudumia wagonjwa 558, kati yao 274” alisema Pro Museru.
 • Akasema, wagonjwa walikuwa na uvimbe wa kinywa na  gharama yake ikiwa TZS Bil.2.192, sawa TZS milioni 8 kwa mgonjwa mmoja, akaongeza kuwa iwapo wagonjwa wangepelekwa Nje ya Nchi serikali ingetumia TZS Bil.26.304, sawa na TZS Milioni 96 kwa mgonjwa mmoja.
22-01
Mashine ya Maabara
 • Mafanikio mengine aliyataja kuwa ni upatikanaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini ambapo wagonjwa 380 walipata huduma  kwa gharama ya TZS Mill. 116, 820, 000, huku huduma hiyo ikipatikana kwa TZS Bil.1, 514, 270, 00 na hivyo hospitali imeokoa TZS Bil.1, 397, 450, 000
 • Serikali pia imeboresha mazingira ya kazi ambapo TZS Bil.10, 041, 118, 424.84, zimetumika kwa kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka vyumba 13 hadi 20 na ukarabati wa vyumba hivyo uko tayari, na umegharimu TZS Bil.2.46, vyumba vya wagonjwa mahututi ICU  ya watoto wachanga (NICU) yenye vitanda 10 kwa TZS Bil.2.6, ICU ya watoto kuanzia Mwezi mmoja  PICU vitanda 12 kwa gharama ya TZS Bil.2.3,
111-01
Mashine yakuweka dawa ya usingizi kwenye chumba cha upasuaji
 • Vingine ni ICU ya wagonjwa wa Tiba MICU vitanda 15, ya wagonjwa wa upasuaji vitanda 18, ya wagonjwa wanaopandikizwa figo vitanda 5 pamoja na ICU ya wamama wajawazito vitanda 10,  ambapo ujenzi na ukarabati wake umegharimu TZS Mil.614.2.
 • Hospitali imepiga hatua kubwa kwenye mabadiliko, ambayo yanafanywa na Serikali na inafahamika huduma kubwa ambazo awali zilikuwa zikitolewa kwa gharama kubwa, sasa zinapatikana kwa gharama nafuu baada ya Serikali kuwekeza sekta ya Afya kwenye Miaka hii minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *