EURO MILIONI 140 ZA ACP KUWANUFAISHA WAKULIMA WA MAHINDI NA KOROSHO

  • Jumla ya Euro milioni 140 zimetengwa ili kuwanufaisha wakulima wa mazao ya korosho na mahindi katika mpango maalum wa kutoa mikopo,kujenga uwezo katika uzalishaji,masoko,uwekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao hayo kwa wakulima wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific jambo litakalosaidia kupunguza umasikini na njaa katika nchi hizo.
  • Akizungumza katika mkutano wa 110 wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific uliofunguliwa na makamu wa rais wa Kenya Mhe. William Ruto jijini Nairobi nchini Kenya,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Tanzania imetoa hoja ya kutaka mazao ya korosho na mahindi kuongezwa katika mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP jambo ambalo limeridhiwa na kuungwa mkono nan chi za Benin na Burkinafaso.
  • Ameongeza kuwa kukubalika kwa hoja hiyo iliyowezesha mazao hayo kuingizwa katika moja ya mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP Serikali ya Tanzania itajipanga kupitia wizara husika ili kuandaa mapendekezo ya namna ambayo wakulima wa Tanzania watanufaika na program hiyo sambamba na mazao mengine yakiwemo pamba,miwa na kahawa.
  • Aidha,Waziri Kabudi amesema kuwa kupitia program hiyo maalum ya ACP  wakulima wa korosho na mahindi watawekewa mikakati ya kusaidiwa katika uzalishaji,kutafutiwa masoko na mbinu za uwekezaji sanjari na kuongeza mnyororo wa  thamani na kusaidiwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kuathiri uzalishaji wa mazao hayo.
  • Program hiyo ya ACP imetajwa kuwa mkombozi kwa nchi hizo katika jitihada za kupunguza umasikini na ukosefu wa chakula kwa kuwa  unalenga zaidi wakulima wa chini na wa kati hususani wanawake na vijana.
  • Mazao mengine yaliyopo katika mpango wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific kwa muda mrefu sasa licha ya kuwa Tanzania haijatumia fursa hiyo kikamilifu ni pamoja na Pamba,kahawa na cocoa kwa nchi nyingi za Afrika nan dizi,miwa,kava na raum kwa nchi za Caribbean na Pacifiki.
  • Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Kenya Balozi Pindi Chana amesema Ubalozi wa Tanzania Nchini humo unafuatilia kwa ukaribu mkutano huo kwa kuwa utatoa fursa mbalimbali ambazo zitaiwezesha Tanzania kunufaika nazo hususani kupitia mazao ya kilimo jambo ambalo litasaidia kupunguza umasikini na ukosefu wa ajira hususani kwa akina mama na vijana.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA KOROSHO WA MKOA WA LINDI NA MTWARA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *