NCHI ZA ACP ZATAKA MAJADILIONO UPYA KUHUSU MKATABA WA EPA

  • Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) Tanzania ikiwemo zimekubaliana kuwa nchi za ACP na Umoja wa Ulaya zifanye maridhiano katika maeneo yanayoonekana kuwa ni kikwazo kwa baadhi ya nchi hizo kutosaini  mkataba wa EPA ama kuitekeleza.
  • Azimio hilo la Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific zimefikia makubaliano hayo katika mkutano wa 110 wa nchi hizo unaoendelea jijini Nairobi nchini Kenya.
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema nchi hizo zimekubaliana kufanya mapitio mapya ya mikataba ya EPA uliyoingia na nchi za ACP.
  • Ameongeza kuwa mapitio hayo yanalenga kuzingatia hali halisi ya sasa duniani ikiwa ni pamoja na Malengo ya Dunia ya Maendeleo Endelevu, Makubaliano ya Mkataba wa Paris kuhusu Mazingira na uhalisia mwingine ndani na nje ya Umoja wa Ulaya.

  • Aidha maazimio mengine yaliyopitishwa katika mkutano huo wa 110 wa Baraza la mawaziri wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) ni pamoja na kuifanya ACP kuwa umoja wa kisasa zaidi katika malengo yake, muundo wake na mikakati yake katika kufikia ACP tunayoitaka (The ACP we want) ikiwa ni pamoja na kubadilisha jina kutoka KUNDI la ACP na kuwa UMOJA wa ACP, yaani kutoka African Caribbean and Pacific Group of States (ACP Group of States) na kuitwa Organisation of the African Caribbean and Pacific Group of States (OACP group of states).
  •  Prof. Kabudi amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuifanya ACP kuwa na nguvu zaidi katika kupanga, kuweka mikakati na kutekeleza kwa ufanisi malengo ya Umoja wetu.
  • Pia baraza limefanya uamuzi wa kumchagua Balozi George Rebelo Pinto Chikoti kutoka Jamhuri ya Angola kuwa Katibu Mkuu wa Sekretariati ya ACP kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.
  • Kuhusu suala la kujitegemea Baraza limeidhinisha uamuzi wa kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa jumuiya ya kundi la nchi za Afrika Caribbean na Pasific kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya utegemezi katika kuendesha jumuiya. mfuko huu utaweza kufanya uwekezaji kwa kutumia fedha za Umoja pamoja fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali badala ya kutegemea zaidi ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya.
  • Katika mkutano huo Tanzania imeweza kufanya majadiliano ya pembezoni na Jamhuri ya Kenya ambaye ni nchi mwenyeji wa mkutano 110 wa nchi wanachama wa Afrika,Caribbean na Pacific na hatimaye kukubaliana kuwasilisha pendekezo ambalo limepitishwa na Baraza la Mawaziri la kutumia maneno ya kiswahili katika kaulimbiu ya Azimio la Nairobi ambayo inaiitwa “NAIROBI NGUVU YA PAMOJA DECLARATION”. Hatua hii ni sehemu ya kuenzi na kukuza Kiswahili ndani ya Wanachama wenzetu wa nchi 79 za ACP.
  • Jumatatu ya Desemba 09,2019 mkutano huo unaingia katika hatua nyingine ambapo kutafanyika mkutano wa tisa wa wakuu wa kundi la nchi za Afrika,Carribean na Pacific ambapo wakuu wa nchi na serikali wapatao 79 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AMTEUA BALOZI WILBERT IBUGE KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi (Kanali) …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *