SERIKALI INATARAJIA KUJENGA MINARA 5 YA MAWASILIANO WILAYANI MAFIA

  • Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Atashasta Nditiye (Mb.) amezindua mnara wa Mawasiliano katika kijiji cha Chunguruma kilichoko Kata ya Ndagoni Wilaya ya Mafia. Kijiji hicho na maeneo jirani havikuwa na usikivu wa mawasiliano ya simu za mkononi kwa muda mrefu.
  • Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbunge wa Wilaya ya Mafia, Mheshimiwa Mbaraka Dau, ameiashukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza ahadi ya kuhakikisha kijiji hicho na maeneo jirani yanapata huduma za mawasiliano ya simu za mkononi.
2-01
Mnara wenye kasi ya 3G uliojengwa na Serikali kwa kutoa ruzuku kwa Vodacom uliojengwa katika kijiji cha Chunguruna Kata ya Ndagoni Wilaya ya Mafia
  • “Nakushukuru sana Mh. Naibu Waziri kwa kutimiza ahadi ya Serikali kuleta mawasiliano Chunguruma, tufikishie salamu za wananchi wa Mafia kwa Mh. Rais wetu Kipenzi John Pombe Joseph Magufuli kwa kutuletea maendeleo ya Mawasiliano Mafia” alisema Mh. Dau.
  • Mheshimiwa Nditiye akijibu salamu hizo, alisema Serikali kwa kutambua  mawasiliano ni haki ya wananchi na katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliahidi kuhakikisha kila mtanzania anapata mawasiliano.
3-01
Wananchi wa Kijiji cha Chunguruma kilichoko Kata ya Ndagoni wakimsikiliza Naibu Waziri Mh. Atashasta Nditiye (Mb) wakati wa uzinduzi wa mnara wa Mawasiliano kijijini hapo
  • “Rais wetu John  Magufuli anataka kuona Watanzania wote wanapata huduma za mawasiliano kote nchini. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote hatulali usingizi ili kukamilisha kazi hii inakamilika kama ilivyoahidiwa na CCM. Mimi jukumu langu ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za simu kwa mawasiliano na huduma za kutuma na kupokea miamala ya fedha na kufanya malipo kupitia teknolojia ya mawasiliano”, alisema Mheshimiwa Nditiye.
4-01
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mh. Shaib Mnunduma akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bibi Jestina Mashiba kwa kufanikisha kujengwa kwa Mnara wa Mawasiliano kijijini Chunguruma kata ya Ndagoni Mafia. Anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Dr. Jim Yonazi na mjumbe wa Bodi ya UCSAF Bibi Eunice Masigati
  • Mwaka jana 2019 mwezi mei, Mh Nditiye alifanya ukaguzi wa usikivu wa huduma za mawasiliano na kubaini eneo la Chunguruma halikuwa na huduma ya mawasiliano ya kuridhisha. Aliuagiza Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kujenga mnara kwa kushirikiana na kampuni ya simu. Vodacom Tanzania ilishinda tenda ya kujenga mnara huo wenye uwezo wa 3G na umeanza kufanya kazi, na wananchi wa maeneo ya Ndagoni na maeneo ya jirani wanapata mawasiliano ya uhakika sasa.
5-01
5. Mbunge wa Mafia Mh. Mbaraka Dau akiongea katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa Mawasiliano kijijini Chunguruma, Mafia
  • Awali Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Shaib Mnunduma aliishukuru Serikali kwa kujenga mnara huo ambao utasaidia wananchi kuwasiliana na kupata huduma za dharura hasa wavuvi wanapokuwa baharini. “Kumekuwa na dharura nyingi sana kwa wavuvi wetu na wanapata shida ya kupata huduma za uokozi kwa kukosekana kwa mawasiliano.
6-01
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mh. Shaib Mnunduma akimshukuru Mh. Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano kwa kutimiza ahadi ya kujengwa kwa Mnara wa Mawasiliano kijijini Chunguruma kata ya Ndagoni Mafia alipotembelea Wilaya hiyo mwezi Mei 2019. Mnara huo uliojengwa na Mfuko wa Mawasilano kwa Wote kwa kutoa ruzuku kwa VODACOM umezinduliwa jumamosi tarehe 1, 2020.
  • Akizungumza na wananchi wa Chunguruma, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Bibi Justina Mashiba amewahakikishia viongozi na wananchi wa Wilaya ya Mafia kuwa changamoto za mawasiliano katika Wilaya ya Mafia zitaisha na kwa sasa Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Uua miradi ya kujenga minara 5 ya Mawasiliano katika Wilaya hiyo hivi karibuni kwenye maeneo mengine yenye tatizo la usikivu wa mawasiliano.
7-01
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chunguruma, Ndagoni Mafia alipokwenda kuzindua mnara wa Mawasiliano uliojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

 

 

 

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUPELEKA MAWASILIANO YA SIMU SINGIDA MASHARIKI

Serikali imeahidi kujenga mnara wa simu katika Kijiji cha Msule kilichopo kata ya Misugha jimbo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *