SERIKALI KUPELEKA MAWASILIANO YA SIMU SINGIDA MASHARIKI

 • Serikali imeahidi kujenga mnara wa simu katika Kijiji cha Msule kilichopo kata ya Misugha jimbo la Singida Mashariki ili kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto iliyopo.
 • Kufuatia ahadi hiyo imelielekeza Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL)kujenga mnara huo na kuhakikisha hadi Agosti mwaka huu wawe wamewasha rasmi mawasiliano.
S7-01
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa jimbo la Singida Mashariki
 • Agizo hilo linafuatia ombi la mbunge wa jimbo hilo Miraji Mtaturu  aliyeiomba serikali kupeleka mawasiliano ya simu kwa wananchi.
 • Akizungumza katika ziara yake ya kikazi jimboni humo ,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano mhandisi Atashasta Nditiye amesema serikali imesikia kilio cha wananchi kupitia ombi la mbunge hivyo ni ahadi yao kwao kuwa watajibu ombi hilo kwa wakati.
S6-01
Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu  akizungumza na wananchi wa jimbo la Singida Mashariki wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye
 •  “Ilani yetu ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)imeelekeza serikali kuhakikisha inafikisha mawasiliano kwa wananchi,na serikali yetu chini ya Rais Dokta John Magufuli ni sikivu,hivyo niahidi kwenu kuwa changamoto hii itapatiwa ufumbuzi,”alisema Mhandisi Nditiye.
 • Awali akitoa ombi hilo Mtaturu amesema wananchi wa Kata za Misughaa,Kikio na Ntuntu wanachangamoto kubwa ya mawasiliano ya simu hivyo ni matarajio yao kuwa ombi hilo litasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.
S5-01
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa jimbo la Singida Mashariki
 • “Mheshimiwa naibu waziri juzi nilikuomba uje ujionee hali ya wananchi wangu ilivyo katika sekta ya mawasiliano,na nashukuru umekubali wito wangu umefika na umeshuhudia simu ulizokuwa nazo mwenyewe hazisomi mtandao wowote,kwa niaba ya wananchi hawa naomba tujengewe mnara ili kurahisisha mawasiliano ya kibiashara na kijamii kwani  mawasiliano ndio kichocheo kikubwa cha maendeleo,”alisema Mtaturu.
 • Aidha upande wa barabara ameiomba serikali kutenga fedha ili kujenga barabara ya Njia panda Singida kupitia kwa mtoro hadi Kiblashi Tanga yenye urefu wa kilomita 461 kwa kiwango cha lami.
S2-01
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye akizungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu
 • “Tangu mwaka 2017 serikali imemaliza kufanya upembuzi yakinifu kwenye barabara hiyo,tunachoomba sasa ni kutengwa kwa fedha ili barabara hiyo ijengwe kwa kuwa ni muhimu kiuchumi kutokana na kugusa mikoa mitatu ya Dodoma,Singida na Tanga,”aliongeza Mtaturu.
 • Mbali na maombi hayo amemshukuru Rais Dokta John Magufuli kwa kupeleka fedha nyingi katika miradi mbalimbali kwenye sekta ya elimu,afya na miundombinu ya mawasiliano katika maeneo mengine ya jimbo hilo
 • Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo ameeleza umuhimu wa mawasiliano kiusalama na katika kuchochea maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
S1-01
Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu  akizungumza na wananchi wa jimbo la Singida Mashariki wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye
 • “Kwanza nikushukuru Mbunge kwa kumualika kiongozi wetu aje ajionee kwa macho changamoto iliyopo kwenye wilaya yetu,ila tu nikuombe mbali na maeneo uliyoyataja,utusaidie pia kwenye maeneo mengine kama ya Ighombwe,Mgungira na Iyumbu ambako nako pia mawasiliano ni shida,”alitoa ombi Mpogolo.
 • Katika ziara hiyo mhandisi Nditiye ametoa Printer moja kwa shule ya sekondari ya Dokta Shein na kuahidi kutoa computer tano ambapo kila shule ya sekondari wilayani humo itapata computer moja ambayo itaunganishwa na internet ili itumike kufundisha kwa njia ya masafa,msaada ambao umeahidiwa pia na mbunge Mtaturu.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI INATARAJIA KUJENGA MINARA 5 YA MAWASILIANO WILAYANI MAFIA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Atashasta Nditiye (Mb.) amezindua mnara wa Mawasiliano …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.