WAZIRI MWAKYEMBE AWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA MICHEZO

  • Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kujitokeza kuchangia ujenzi wa viwanja vya michezo ambavyo vitasaidia katika kuibua vipaji vya michezo kwa vijana.
  • Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo bungeni Jijini Dodoma alipokuwa kijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Cecilia Pareso (CHADEMA) lilohoji kwanini serikali isijenge Sports Area katika Miji mikubwa kwani kupitia viwanja hivyo kutasaidia kuibua vipaji vingi zaidi kama vya akina Mbwana Samatta ambao watalitangaza taifa vyema.
  • ‘’Suala la kujenga viwanja vya michezo si la serikali pekee ni pamoja na wadau wote na kwa sasa kuna mtanzania mmoja aishie Marekani ambaye amejenga uwanja wa michezo mzuri Mkoani Arusha katika eneo la Sekei ambao kwa sasa umekwisha fikia asilimia 90, pia Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha nayo imejenga Sports Arena katika eneo la Ngarenaro hizi zote ni jitihada mbalimbali za kukuza sekta ya michezo na kuibua vipaji,’’alisema Dkt.Mwakyembe.
  • Swali hilo liliibuka baada ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mheshimiwa Juliana Shonza kutoa mjibu ya swali la msingi la Mbunge wa Kinondoni Mhe.Maulid Said Mtulia (CCM) lilohoji  serikali inampango gani katika kuimarisha sekta ya michezo kwa kuandaa wakufunzi wa michezo,kujenga viwanja vya kisasa,kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya michezo ambapo Naibu waziri huyo alijibu kuwa  serikali kupitia Chuo cha Michezo Malya kilichopo Mkoani Mwanza kinatoa kozi mbalimbali katika ngazi ya Stashahada, Diploma in Sport Administration and Couching ambayo hutolewa kwa miaka miwili.
  • ‘’Katika kuimairisha sekta ya michezo serikali imeendelea kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusu taaluma tofauti za michezo kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na elimu ya michezo hutolewa katika ngazi ya Shahada kupitia Idara Maalumu ya Physical Education and Sports Science (PESS),’’alisema Mhe.Shonza.
  • Pamoja na hayo Mheshimiwa Shonza aliendelea kusisitiza kuwa suala la ujenzi wa miundombinu ya viwanja si la wizara peke yake nilawatanzania wote ikiwemo sekta binafsi pia katika kuhakikisha upatikanaji rahisi wa vifaa vya michezo serikali imekuwa ikihamasisha wadau mbalimbali kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya vifaa vya michezo pamoja wafanyabiashara kuleta vifaaa vya michezo nchini ilikurahisisha upatikanaji wa vifaa hivyo.Na Anitha Jonas – WHUSM
Ad

Unaweza kuangalia pia

KATIBU MKUU DKT. ABBASI ASISITIZA MAGEUZI YA KIUTENDAJI KWA MENEJIMENTI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi amewataka viongozi wa menejimenti wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *