Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini ya dhahabu nchini umeshika kasi huku ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2020 na kuifanya dhahabu ya Tanzania kusafirishwa ikiwa tayari imechakatwa na hivyo kuongeza thamani ya madini hayo katika soko la dunia.
Ujenzi wa kiwanda hicho ulianza rasmi mwezi Machi, 2020 ambapo ujenzi wake mpaka sasa umefikia asilimia 40, imeelezwa kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho utapelekea suala la kisheria la kutokusafirisha madini ghafi kutekelezwa ipasavyo.
Hayo yalibainishwa Mei 12, 2020 wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa kiwanda hicho na taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho unaoendelea kwa kasi mkoani Mwanza kutolewa.
Akizungumzia mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017, Naibu Waziri Nyongo alisema, kukamilika kwa kiwanda hicho kutakwenda sanjari na sheria inayowataka wafanyabiashara wa madini kutokusafirisha madini ghafi na badala yake madini yote kusafirishwa yakiwa yamechakatwa na kuongezewa thamani itakayopelekea kuuzwa kwa bei nzuri katika soko la Dunia.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika eneo hilo la ujenzi, Naibu Waziri Nyongo alikiri kufurahishwa na usimamizi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kasi ya mkandarasi anayesimamia ujenzi wa kiwanda hicho na kukiri kuwa Serikali itakuwa ikitembelea eneo hilo mara kwa mara ili kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa wakati na kiwanda kufunguliwa kwa wakati kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt.Venance Mwasse ameeleza kuwa ukamilishwaji wa mradi huo utakwenda sambamba na mradi wa kuwawezesha wachimbaji wadogo katika suala zima la kusafisha dhahabu waliyochimba katika maeneo yao.
Aidha, Dkt. Mwasse amesema msaada utakaotolewa kwa wachimbaji wadogo kutasaidia kiwanda hicho kupata malighafi zakutosha kwa ajili ya kulisha kiwanda kinachotarajiwa kuzalisha kilo 480 za dhahabu kwa siku yenye purity ya kiasi cha 999.99 ambacho ni kiwango cha juu kabisa cha purity ya dhahabu duniani.
Mollan SP, Chong YJ, Grech O, Sinclair AJ, Wakerley BR cialis with priligy Martha Libster, PhD c