KILIMO CHA UMWAGILIAJI KIMEONGEZA UZALISHAJI WA MPUNGA TOKA WASTANI WA TANI 4.0 MWAKA 2014 HADI TANI 7.2 KWA MWAKA 2019

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya amewaeleza wahandisi wa umwagiliaji mikoa kuwa wana deni la kurejesha imani kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi yenye ubora na tija ya uzalishaji mazao ya wakulima kwa kuwa fedha nyingi za umma zinatumika.

Katibu Mkuu amesema hayo mkoani Morogoro alipokutana na Wahandisi wa umwagiliaji mikoa, na kutoa wito kwa waandisi hao kufanya kazi kwa bidii ili kutimza malengo ya serikali katika kukuza kilimo cha umwagiliaji

Ad

“Chama cha Ushirika wa Wakulima Wadogo Wadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWAKUDA LTD) kimeongeza uzalishaji mpunga toka wastani wa tani 4.0 mwaka 2014 hadi tani 7.2 kwa hekta mwaka 2019 kufuatia serikali kuboresha miundombinu ” amesema Gerald Kusaya KM Kilimo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *