Maktaba ya Mwaka: 2020

PROF. SHEMDOE AILEKEZA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA BIDHAA ZA VIWANDA KILA ROBO YA MWAKA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelezo ya ufafanuzi muda mchache baada ya ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini,  05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere – Dar es Salaam. …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA HOSPITALI YA UHURU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua umaliziaji wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru unaoendelea katika wilaya ya Chamwino, Dodoma na kuagiza huduma zianze kutolewa ifikapo Desemba 20 mwaka huu. Amekagua hospitali hiyo (Jumapili, Desemba 6, 2020) na amesema vifaa vyote zikiwemo samani, vifaa tiba vinavyotakiwa kuwepo kwenye hospitali hiyo vipelekwe na …

Soma zaidi »

TANZANIA YAUNGA MKONO AZIMIO LA AU KUONGEZA MIAKA 10 YA KUONDOA NA KUTOKOMEZA SILAHA HARAMU

Umoja wa Afrika (AU) umezitaka nchi wanachama wa umoja huo kutilia mkazo azimio la kuondoa na kutokomeza silaha haramu ili kuliondoka na migogoro inayolifanya bara hilo kushindwa kusonga mbele kiuchumi. Akifungua Mkutano wa 14 wa dharura wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia ya mtandao (virtual Conference) Mwenyekiti wa Umoja …

Soma zaidi »

WAWEKEZAJI MAKAMPUNI 13 KUTOKA NCHINI AUSTRIA WAWASILI DODOMA KUTAFUTA MAENEO YA UWEKEZAJI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha wawekezaji wa makampuni 13 kutoka Austria na Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Kituo cha uwekezaji na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, waliokuja kwa lengo la kutafuta maeneo ya …

Soma zaidi »

“VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO HAVIVUMILIKI TENA” – MGANGA MKUU WA SERIKALI

Na Englibert Kayombo WAMJW – MWANZA Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amesema kuwa Serikali haitovumia tena vifo vya akina mama wajawazito vinavyosababishwa na uzembe wa watumishi kazini. Prof. Makubi ametoa kauli hiyo alipokuwa akifunga kikao kazi cha timu ya uongozi wa afya ya Mkoa wa Mwanza kilichofanyika Wilayani …

Soma zaidi »

DC CHONGOLO: JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA MWANANYAMALA KUANZA KAZI BAADA YA WIKI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Jengo jipya la kisasa la Mama na Mtoto litakalo anza kutoa huduma hivi karibuni. Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua jengo hilo Mhe. Chongolo amesema kuwa jengo …

Soma zaidi »

SERIKALI YAJA NA MFUMO BORA WA HAKIMILIKI KWA WASANII NA WABUNIFU

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ameahidi kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuboresha mifumo ya hakimiliki ili kuhakikisha wasanii wa mawanda mbalimbali wananufaika kila kazi zao za ubunifu zinapotumika iwe kwenye redio, TV, mitandaoni na kila sehemu ya biashara. Dkt. Abbasi …

Soma zaidi »

UJENZI WA KIVUKO CHA MAFIA WAFIKIA ASILIMIA 98 – WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Mv. Kilindoni Hapa Kazi Tu kitakachokuwa kinafanya safari kati ya kisiwa cha Mafia na Nyamisati umefikia asilimia 98 na kwamba ifikapo Desemba 15 mwaka huu kitaingia majini kwa mara ya kwanza. ’’Wana-Mafia tumekuwa tukizungumza sana sasa tumefikia hatua …

Soma zaidi »