KIVUKO CHA MV. MAFANIKIO KUHUDUMIA HADI SAA 2 USIKU BADALA YA SAA 12. JIONI

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jen. Marco Gaguti ametoa agizo la kivuko MV Mafanikio kinachofanya safari zake kuanzia Feri hadi Msangamkuu kuwa kuanzia Oktoba 4, 2021 Kivuko hiko kitahudumia wananchi hadi saa mbili usiku badala ya saa 12 jioni ili kuruhusu wananchi hao kupata muda zaidi katika shughuli zao za kila siku.

Kumekuwa na changamoto ya suala la muda na mmeomba muda uongezwe, tumeridhia kivuko hiki sasa kifanye kazi mpaka saa mbili usiku”Amesema Gaguti

Gaguti ametoa agizo hilo Oktoba 4, 2021 wakati wa mapokezi ya kivuko cha MV. Mafanikio kilipowasili Mkoani Mtwara baada ya kufanyiwa ukarabati ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 493,609,357.70.

Ad

Aidha amewataka wananchi hao kuhakikisha wanalipa kodi kwa usahihi na wakati ili Serikali iweze kuwekeza na kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Mtwara.

“Tujitahidi kulipa kodi hii miradi inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wetu inahitaji uwekezaji wa kutosha, kodi zetu zina tija katika kuleta maendeleo” Amesema Gaguti



Naye Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mkoa wa Mtwara Eng. Japhet Msellu amesema kuwa kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati wa injini na baadhi ya vifaa ambapo matengenezo yote yamegharimu kiasi cha shilingi Milioni 493,609,357.70.

Nae Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassani Mtenga amewataka wananchi kutofanya uharibifu katika miundombinu ya kivuko hicho kwani uharibifu huo utakwamisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.

Bakari Omari Ally mkazi wa Msanga Mkuu ameishukuru Serikali kwa ajili ya ukarabati huo kwani kina usalama zaidi katika matumizi tofauti na mitubwi ambayo inatumika kwa sasa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *