NAIBU WAZIRI KUNDO – SERIKALI INABORESHA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ICT) – Mhe. Mhandisi. Andrea Mathew Kundo amemwagiza Mkuu wa Kanda wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kanda ya Mashariki kushughulikia haraka maombi ya Halmashauri ya Chalinze ya kuimarisha MIundombinu ya mawasiliano ikiwemo kupatiwa kibali cha Masafa ya radio (radio frequency) na Televisheni ambayo yalikwama kwa muda mrefu.

Naibu Waziri Mhandisi Kundo ameyasema hayo Machi Mosi wakati wa ziara maalum aliyofanya katika Halmashauri hiyo ya Chalinze ikiwa ni muendelezo wa ziara yake anayoendelea nayo Nchini kuangalia hali ya mawasiliano nchini.

Ad

Akimkaribisha kuongea na watumishi wa Halmashauri , Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete alimueleza Naibu Waziri kuwa uimara wa mawasiliano ni pamoja na kupata vyombo vya mawasiliano kama Redio na Televisheni ili kuwezesha upashanaji wa habari ya mazuri yanayofanyika katika Wilaya hiyo na hata Tanzania kwa jumla. Katika kuimarisha mawasiliano Mhandisi Kundo amebainisha kuwa, kukosekana kwa radio hiyo inasababisha Wananchi kushindwa kusikia mambo mazuri yanayofanywa na Serikali yao chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

“Wananchi wanataka kusikia mambo yanayofanywa kwenye Halmashauri yao. Pia wanataka kusikia Diwani wao kafanya nini au Mbunge wao kafanya jambo gani ili kupunguza maswali wakati wa kazi au kwenye mikutano ya viongozi wao ama kwa Serikali yao”. Alisema Mhandisi Kundo.

Aidha, Mhandisi Kundo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mbunge wa Chalinze kwa kuwa mtu wa mstari katika kupigania maendeleo ya jimbo hilo. Naibu Waziri alieleza kuwa, alipokea taarifa kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Ridhiwani Kikwete juu ya ombi la uchelewashwaji wa frequency za radio hiyo ya Halmashauri ya Chalinze, hivyo ameamua kutembelea pamoja na shughuli nyengine za kiserikali, kujionea uhalisia sambamba na matatizo mengine ya kimawasiliano.

“Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete aliniuliza juu ya tulipofikia suala lao la radio frequency. Kiukweli suala ili nimelijua jana na leo nimefika hapa hivyo basi ninamwagiza Mkuu wa Kanda wa Mashariki wa TCRA ambaye yupo hapa ahakikishe analifanyia kazi na hadi jioni ya leo niwe nimepata majibu ya kurejesha kwa Mbunge’ alisema Mhandisi Kundo.

Aidha, akijibu suala la changamoto ya upatikanaji hafifu wa mawasiliano baadhi ya maeneo ya Jimbo hilo, Naibu Waziri alibainisha kuwa, kumekuwa na changamoto wa usimikwaji wa minara ya Mawasiliano baadhi ya maeno ikiwemo pia changamoto wa upatikanaji wa vibali.

Na. Andrew Chale, Chalinze

“Vibali vimekuwa vikichukua muda mrefu kuanzia miezi mitatu hadi Sita. Kuna wenzetu wa Mazingira NEMC ambao wao wanachukua hadi miezi Sita, lakini pia Mamlaka ya anga, watu wa hali ya hewa na wadau wengine. Lakini nina hakika masuala haya yatafanyiwa kazi na mawasiliano yatakuwa vizuri” alisema Mhandisi Kundo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete alimshukuru Naibu Waziri kwa kufika jimboni Chalinze pamoja na kukubali maombi yao ya kuhakikishiwa mazingira bora ya mawasiliano. Pamoja na kumshukuru Naibu Waziri, Mbunge Kikwete alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Magufuli kwa kuchagua viongozi wachapa kazi kama Mhandisi Kundo ambaye amekuwa akifika majimboni kutatua kero za wananchi.

“Mhe. Naibu Waziri leo umekuja hapa Jimboni utatupatia mwanga mpya kupitia mawasiliano yetu. Jimbo letu limekuwa na shida katika mawasiliano kwa muda mrefu matatizo ambayo yana sura zinazofanana katika utatu wake. Akieleza juu ya shida hiyo Mbunge Kikwete alitoa mfano wa kijiji cha Matipwili na Kijiji cha Mkoko , Mheshimiwa Mbunge alieleza shida kubwa ya vijiji vyote zinafanana ambapo mitambo hiyo uzimwa inapofika saa mbili au nne usiku hivyo wananchi kukosa mawasiliano usiku. Akijibu Meneja wa Kampuni ya Tigo ambao ndiyo wanaosimamia mradi huo alikiri juu ya tatizo hilo lakini sasa limerekebishwa kwa kurekebisha miundombinu na mazingira ya kuwapatia wananchi mawasiliano.

Pamoja na hilo Mbunge alieleza matatizo mengine yakiwemo yale ya mawasiliano kukosekana barabarani kati ya kijiji na kijiji au miji na miji mfano kijiji cha Kwa Mduma na Kitongoji cha Gole, Alibainisha Mbunge Ridhiwani Kikwete. Akijibu Naibu Waziri alimuhakikishia Mbunge na wananchi wa Chalinze kuwa serikali inaangalia pia thamani ya biashara na kupitia Mfuko wa mawasiliano kwa Umma mapungufu kama haya yanaangaliwa.

Mapema, kabla ya Ujio wa Naibu Waziri , Halmashauri ya Chalinze ilipokea Vifaa vya kupimia Ardhi ili kuwezesha upimaji wa Viwanja na kupanga miji ya Halmashauri ya Chalinze.

Wakipokea vifaa hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ndg. kamugisha alishukuru ununuzi wa Vifaa na kwamba unaleta ukombozi mpya kwa Chalinze huku Mbunge akishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kutekeleza maagizo ya Baraza la Madiwani na maagizo ya Viongozi.

Vifaa hivi vinasaidia kurahisisha Upimaji. Vifaa hivi vitawezesha kwa siku kupimwa kwa viwanja hadi 200 toka utaratibu wa kawaida wa viwanja 5.

Ad

Unaweza kuangalia pia

TRENI YA MCHONGOKO YAANZA SAFARI KWA KISHINDO DAR – DOM

Treni ya Umeme ya Kisasa (EMU) ya Reli ya Kisasa (SGR) nchini Tanzania ni sehemu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *