KENANI AKAGUA MRADI WA MAJI WA BILIONI 520

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi amefanya ziara ya kikazi Kukagua mradi wa Maji wa Bilioni 520 akiambatana na Madiwani wa jiji la Arusha wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximillian Iraghe pamoja na watendaji wa kata katika Jiji la Arusha.

Mkuu wa Wilaya amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi na kwa sasa upo hatua nzuri na kusema kuwa Serikali ipo kazini kuhakikisha maendeleo makubwa yanawanaufaisha wananchi.

Ad

Mkuu wa Wilaya amewapongeza Mamlaka ya Maji AUWSA na kuwaagiza wakamilishe mradi kwa wakati ili Wananchi waanze kupata maji safi na salama.





Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Tanzania na Czech Zakubaliana Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili

Serikali za Tanzania na Czech kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kuvutia uwekezaji kati yao. Kuondoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *