Taarifa ya Habari

PSSSF YATUMIA BILIONI 880 KULIPA MAFAO

Wanachama elfu kumi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamelipwa takribani Bilioni 880/- ikiwa ni malimbikizo ya Pensheni kwa wastaafu  tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo mapema mwaka jana. Akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dodoma Meneja Kiongozi, Uhusiano  wa mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema kuwa dhamira …

Soma zaidi »

WAZIRI JAFO AKABIDHI BIL 1.7 RUZUKU KWA VIJANA TOKA USAID

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo  amekabidhi hundi za mfano zenye thamani ya Tsh 1,731,038,850 kwa Taasisi tisa za vijana wa Mikoa ya Mbeya, Iringa pamoja na Zanzibar kwenye hafla ya iliyofanyika kwenye viwanja vya Sido Jijini Mbeya. Akizungumza katika hafla …

Soma zaidi »

ALMASI YENYE THAMANI YA BILIONI 3.2 YAIPAISHA SEKTA YA MADINI TANZANIA

Tanzania imetajwa kuweka historia katika tasnia ya madini baada ya Almasi yenye Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika eneo la Maganzo Mkoani Shinyanga  na kuuzwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2. Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusiana na madini hayo,Naibu  Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus  Nyongo amesema kuwa  kutokana na kupatikana …

Soma zaidi »

MRADI WA RELI YA KISASA (SGR), MWAMBA WA CHANGAMOTO ZA USAFIRISHAJI NCHINI

Na. Paschal Dotto-MAELEZO Ni Takribani Miaka 120 ambapo historia iliandikwa, mwaka 1912, Serikali ya Kikoloni nchini iliamua kuimarisha sekta ya usafirishaji Kwa kujenga Reli, ambapo njia zake ziliunganisha Miji hasa maeneo ya kilimo, uzalishaji na kibiashara, reli kuu kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, hatimaye Kigoma na Tanga. Ni dhahiri …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME SAMUNGE NA DIGODIGO WILAYANI NGORONGORO

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasha umeme katika Vijiji vya Samunge na Digodigo vilivyopo wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kumtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini wilayani humo kuongeza kasi zaidi. Akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme wilayani humo, Waziri Kalemani …

Soma zaidi »

SERIKALI YAJIPANGA KUUNGANISHA GESI ASILIA MAJUMBANI NCHI NZIMA

Serikali imesema Mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ni endelevu na utafanyika katika mikoa yote nchi nzima awamu kwa awamu. Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, alibainisha hayo jana, Mei 25, 2019 jijini Dodoma katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ambayo ililenga kuwajengea …

Soma zaidi »