WAZIRI JAFO AKABIDHI BIL 1.7 RUZUKU KWA VIJANA TOKA USAID

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo  amekabidhi hundi za mfano zenye thamani ya Tsh 1,731,038,850 kwa Taasisi tisa za vijana wa Mikoa ya Mbeya, Iringa pamoja na Zanzibar kwenye hafla ya iliyofanyika kwenye viwanja vya Sido Jijini Mbeya.
  • Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Jafo amesema Ruzuku hiyo inayotolewa kwa mara ya pili sasa  itawezesha vijana kupewa ujuzi utakaowasiaidia katika kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hatimaye maendeleo  ya Taifa kwa ujumla.
jaf-1-01
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akikabidhi hundi ya mfano kwa Taasisi ya Iringa Mercy Organisation wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku inayotolewa na mradi wa Inua Vijana iliyofanyika kwenye viwanja vya Sido Jijini Mbeya.
  • “Fedha hizi zinztolewa kama Ruzuku kupitia kwa Taasisi Tisa ambazo zitafanya kazi mbalimbali ili kuwafikia vijana wa maeneo yote ambao mradi wa Inua Vijna unatekelezwa hivyo tunataka tuone mabadiliko kwa vijana wetu, tunataka tuone maendeleo ya moja kwa moja kupitia fedha hizi.
  • Ni vyema sasa Mradi wa Inua Vijana mkafanya tathmini ya kina kuona ni namna gani fedha hizi zinaleta mabadiliko yenye Tija kwa vijana wetu, uchumi wao umeimarika kwa kiasi gani na kama kuna sehemu ambayo bado inahitaji ufadhili nguvu zielekezwe zaidi kwenye eneo husika ili matokeo ya haraka yaweze kupatikana” Alisema Jafo.
  •  Vijana wa sasa wanatakiwa kujengewa mawazo mapana zaidi, kupewa ujuzi utakaowezesha kuwa wabunifu na kufanya shughuli ambazo zitawaingizia kipato kikubwa cha kuwafanya kutoka kwenye kipato cha chini na kuwa watu wenye kipato cha kati Aliongeza Jafo.
JAFO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo kikabidhi hundi ya mfano kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Baba Watoto Oscar Kapande inayofanya shughuli zake Wilayani Kilolo Mkoani Iringa.
  • “Mradi huu ni muhimu sana kwa mendeleo ya Taifa letu kwani unalenga kukuza uchumi, kupunguza umasikini na kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi kwa kuhakikisha kuwa sekta zinazogusa maisha ya watu wengi na maskini zinakuwa kwa kasi” Alsiema Jafo.
  • Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ndiye mwejeji wa hafla hii Albert Chalamila alisema ni katika Mkoa wa Mbeya mradi wa Inua Vijana umefanikwa kubadilisha maisha ya vijana wengi ambao wamejengwa uwezo katika maeneo ya ujasiriamali, uongozi afya ya uzazi pamoja na kupewa ujuzi katika kazi mbalimbali za kuwaingizia kipato.
  • “Ukishindwa kumshukuru binadamu mwenzio hata Mungu sio rahisi kumshkuru mimi napenda niwashkuru sana USAID kupitia mradi wa Inua Vijana kwa kazi kubwa waliofanya katika Mkoa wangu wa Mbeya tunatambua mchango wenu na pia niombe mzidi kuwafikia vijana wengine kwenye Wilaya ambazo mradi huu haujafika ili nao wanufaike na matunda haya” Alisema Chalamila.
JAFO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku inayotolewa na mradi wa Inua Vijana iliyofanyika kwenye viwanja vya Sido Jijini Mbeya.
  • Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happy ambaye Mkoa wake ni wanufaika wa mradi wa Inua Vijana alisema kuwa ukiwawezesha vijana umewezesha Taifa kwa kuwa vijana ndio Nguvu kazi ya Taifa nafurahia kuona mafanikio ya mradi huu kwenye Mkoa wangu na mi ntazidiki kutoa ushirikiano kila itakapohitajika ili vijana wa Kitanzania wazidi kupata hii fursa.
  • Aidha Mhe. Happy alisema, Miradi hii ya vijana ili iwe na Tija lazima iwe endelevu ni bora pale mradi unapoisha zile rasilimali za mradi zitakakabidhiwa kwa vijana ili waendelee kuzitumia katika kuendeleza miradi hii ambayo imeanzishwa.
  • Mkurugenzi wa  Mkaazi wa USAID Tanzania Andy Karas alisema zoezi la kukabidhi ruzuku kwa ajili ya vijana linafanyika kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza zaidi ya shilingi Bil 1 zilitolewa lengo ikiwa ni kuwaunganisha vijana na fursa mbalimbali za ujasiriamali na ajira kwa kuzingatia mnyororo wa thamani katika sekta za kilimo na mifugo.
  • Naye Mtaalam wa Vijana kutoka USAID Joyce Mndambi amesema kuwa mradi huu una nia ya kubadilisha mtazamo na matarajio ya vijana kwa kuwaendeleza katika fani mbalimbali zikiwemo ujasiriamali, uongozi na kuimarisha Afya zao.Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Ad

Unaweza kuangalia pia

TUMEDHAMIRIA KUONGEZA WIGO UPASUAJI – DKT. KAJUNGU

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mkoani kilichopo mkoani Pwani katika Halmashuri ya Kibaha Mji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *