Taarifa ya Habari

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YATAKIWA KUJIUNGA NA TIBA MTANDAO

Hospitali ya Benjamin Mkapa imetakiwa kujiunga na tiba mtandao ili kuweza kutoa tiba kwa wagonjwa kwa haraka na kwa ufanisi ili kuwapunguzia wagonjwa muda wa kusubiri majibu hususani ya mionzi Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipoitembelea hospitali hiyo …

Soma zaidi »

SERIKALI YAJIZATITI KUIMARISHA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA RASILIMALI MADINI

Serikali imedhamiria kuwa na mikakati endelevu ya kusimamia na kudhibiti rasilimali madini ili ilete tija iliyokusudiwa kwa Taifa. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) leo Januari 25, 2020 Jijini Dodoma alipokuwa akifungua kikao …

Soma zaidi »

OFISI YA MAKAMU  WA RAIS KWA KUSHIRIKIANA NA UNIDO WAANDAA WARSHA YA MAFUNZO

Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani (UV-B) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali. Tafiti zimethibitisha kuwa kumong’onyoka kwa tabaka la ozoni kumetokana na kurundikana  angani kwa kemikali/gesi zinazotumika kwenye mafriji, viyoyozi na mitambo ya kupoozea joto. …

Soma zaidi »

NENDENI MKACHAPE KAZI KWA UADILIFU NA KUTANGULIZA MASLAHI YA TANZANIA – RAIS MAGUFULI

Rais  Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 27 Januari, 2020 amewaapisha Mawaziri 2 na Mabalozi 3 aliowateua hivi Karibuni. Mawaziri walioapishwa ni George Boniface Mwataguluvala Simbachawene aliyeapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na  Mussa Azzan Zungu aliyeapishwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na …

Soma zaidi »

KINU CHA KUFUA HEWA KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI

Imeelezwa kuwa uwepo wa kinu kipya na cha kisasa chenye uwezo wa kufua hewa ikiwemo hewa safi ya Oxygen na ile ya Naitrojeni kitakuwa msaada kwa wenye tatizo la uzazi nchini. Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya kaskazini (KCMC) imesema kuwa, wananchi watapata msaada huo kwani watakuwa na uwezo wa …

Soma zaidi »

HOSPITALI YA MAWENZI YAWAFANYIA UPASUAJI WA JICHO WAGONJWA 640

Kufuatia maboresho mbalimbali katika Sekta ya Afya hapa Nchini Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ya Mkoa wa Kilimanjaro imeweza kufanya upasuaji wa kuondoa ukungu wa jicho kwa wagonjwa 640. Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto …

Soma zaidi »

SERIKALI KUPELEKA MAWASILIANO YA SIMU SINGIDA MASHARIKI

Serikali imeahidi kujenga mnara wa simu katika Kijiji cha Msule kilichopo kata ya Misugha jimbo la Singida Mashariki ili kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto iliyopo. Kufuatia ahadi hiyo imelielekeza Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL)kujenga mnara huo na kuhakikisha hadi Agosti mwaka huu wawe wamewasha rasmi mawasiliano. Agizo hilo linafuatia ombi la …

Soma zaidi »

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LA PITISHA BAJETI YA BILIONI 170.9 KWA MWAKA FEDHA 2020/ 2021

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, katika Mkutano wake maalumu wa Baraza  leo  Alhamisi,  tarehe  23 Januari 2020,   limejadili na  kuidhinisha kwa kauli moja  bajeti yake ya  Tshs  170, 918,524,100/= kwa mwaka wa fedha 2020/2021  ambapo  Tshs.42,951,312, 000/= ni za Mapato ya ndani ya Manispaa na Tshs. …

Soma zaidi »