OFISI YA MAKAMU  WA RAIS KWA KUSHIRIKIANA NA UNIDO WAANDAA WARSHA YA MAFUNZO

  • Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani (UV-B) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali. Tafiti zimethibitisha kuwa kumong’onyoka kwa tabaka la ozoni kumetokana na kurundikana  angani kwa kemikali/gesi zinazotumika kwenye mafriji, viyoyozi na mitambo ya kupoozea joto.
1w-01
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza ambaye ni Mgeni Rasmi katika Warsha ya mafunzo ya kurejeleza gesi zilizotumika na madhara yatokanayo na matumizi ya gesi feki kwa Wakufunzi wa vyuo vya VETA kutoka mikoa yote ya Tanzania akifungua warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na UNIDO.
  • Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi waIdara ya  Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza jijini Dar es Salaama wakati akifungua warsha ya mafunzo ya kurejeleza gesi zilizotumika na madhara yatokanayo na  matumizi ya gesi feki iliyotolewa kwa Wakufunzi wa VETA.
1q-01
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Kemilembe Mutasa akiongea wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi katika Warsha ya mafunzo ya kurejeleza gesi zilizotumika na madhara yatokanayo na matumizi ya gesi feki kwa Wakufunzi wa Vyuo vya VETA Tanzania wanaojihusisha na kuhudumia viyoyozi na mafriji. Warsha hiyo ilifanyika katika Chuo cha VETA- Dar es Salaam.
  • Alisema kuwa Serikali imeaandaa Programu mbali mbali kwa ajili ya utekelezaji wa Itifaki ya Montreal. Mkakati wa kitaifa chini ya mipango ya nchi ni pamoja na: -Kuimarisha uwezo wa Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa Itifaki ya Montreal,  Kukusanya takwimu za uingizaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni, Uhamasishaji juu ya umuhimu wa kulinda tabaka la  ozoni, Kujenga uelewa kwa Wakufunzi juu ya urejelezaji wa gesi iliyokwisha tumika katika mafriji, viyoyozi na mitambo ya kupozea joto, Kuhamasisha matumizi ya kemikali rafiki kwa tabaka la ozoni na  Kuweka utaratibu wa udhibiti wa uingizaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni.
1r-01
Sehemu ya Washiriki wa Warsha ya mafunzo ya kurejeleza gesi zilizotumika na madhara yatokanayo na matumizi ya gesi feki kwa Wakufunzi wa vyuo vya VETA nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha VETA – Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokua yakitolewa katika warsha hiyo.
  • Ofisi ya Makamu wa Rais imekua na utaratibu wa mara kwa mara  kuandaa warsha za mafuzo ya aina hiyo  kwa Wakufunzi wa vyuo vya VETA  Nchini wanaohusika na masuala ya mafriji, viyoyozi na mitambo ya kupoozea joto. Washiriki wa warsha hiyo  wametoka katika vyuo vya VETA vifuatavyo Dar es Salaam, Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mwanza,  Morogoro, Pwani na Kigoma.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *