HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YATAKIWA KUJIUNGA NA TIBA MTANDAO

  • Hospitali ya Benjamin Mkapa imetakiwa kujiunga na tiba mtandao ili kuweza kutoa tiba kwa wagonjwa kwa haraka na kwa ufanisi ili kuwapunguzia wagonjwa muda wa kusubiri majibu hususani ya mionzi
1-01
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kipimo cha uchunguzi wa saratani ya matiti’Mammography’ kilichopo kwenye kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa
  • Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipoitembelea hospitali hiyo kujionea hali ya utoaji huduma.
  • “Nawaelekeza ni vyema mkajiunga na huduma ya tiba mtandao ili muweze kutoa huduma kwa haraka na kwa ufanisi zaidi, mnatakiwa mkajifunze huduma hii kutoka hospitali ya Muhimbili au MOI”. Amesema waziri Ummy.
2-01
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwa kwenye chumba cha kipimo cha CT-Scan kwenye hospitali hiyo
  • Aidha, Waziri huyo amesema kuwa hivi sasa kwenye hospitali nyingi kuna changamoto za wataalam wa kusoma picha kwani wataalam wengi waliopo ni wale wa kupiga ”bahati nzuri sisi tunao wataalam wengi wa kupiga picha mana kwenye mionzi kuna aina mbili za wataalam wapo wa kupiga picha (radiographer) na wa kusoma picha, hivyo serikali itahakikisha inapata wataalam wengi zaidi wa kusoma ili kukidhi mahitaji.
4 -01
Waziri Ummy Mwalimu akiwa kwenye wodi ya wagonjwa walioupandikizaji figo hivi karibuni
  • Waziri Ummy amesema wizara ina lengo la kuziunganisha hospitali za wilaya pamoja na vituo vya afya kwenye mfumo wa hospitali za rufaa za mikoa kwa kufunga senta zitakazosaidia hospitali za wilaya na vituo vya afya vinavyofanya vipimo vya ‘utra sound’ na ‘x-ray’ na majibu yakasomwa haraka na wataalam wa Hospitali za rufaa na kutoa majibu haraka bila kumsubirisha mgonjwa kwa muda mrefu.
5-01
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na watumishi wa hospitali hiyo(hawako puchani)
  • Alitaja hospitali zilizojiunga na tiba mtandao ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa ya Lindi na Morogoro , pia hospitali teule za wilaya za Nyangao,Turiani na hospitali za wilaya ya Nachingwea,kilosa na Mvomero.
6-01
Waziri Ummy akiwa na viongozi wa hospitali hiyo akitembelea maeneo mbali mbali ya utoaji huduma
  • Wakati huo huo Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kupunguza gharama za kulipia uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake kutoka elfu sabini hadi elfu thelathini kama hospitali zingine za taifa zinavyofanya.
7-01
Mmoja wa watoa huduma kwenye idara ya wagonjwa wa dharura akitoa maelezo kwa Waziri wa afya
  • Hata hivyo waziri huyo ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani kutosafiri hadi dar es salaam kupata huduma za kibingwa kwani huduma zote karibu zinapatikana hapo na hivyo ameahidi wizara wataleta madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu pamoja na mifupa. Na. Catherine Sungura – Dodoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI UMMY AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA AFYA ZA WATOTO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wazazi kuwekeza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *