KINU CHA KUFUA HEWA KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI

  • Imeelezwa kuwa uwepo wa kinu kipya na cha kisasa chenye uwezo wa kufua hewa ikiwemo hewa safi ya Oxygen na ile ya Naitrojeni kitakuwa msaada kwa wenye tatizo la uzazi nchini.
  • Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya kaskazini (KCMC) imesema kuwa, wananchi watapata msaada huo kwani watakuwa na uwezo wa kutosha wa kuzalisha hewa hiyo ya Naitrojeni yenye uwezo wa kuhifadhi mbegu za kiume na za kike kwa ajili haswa wenye tatizo la uzazi.
KK2-01
Eneo la kinu hicho cha KCMC
  • Akizungumzia hospitalini hapo ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya yenye lengo la kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uwamu ya tano ndani ya Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Kaimu Mkurugenzi wa KCMC Dkt. Sarah Urasa alisema:
  • “Uhifadhi wa mbegu za kiume na kike upo mbioni kuanza hapo baadae.
  • Hatua hiyo kwani tayari tumeanzisha klininiki maalumu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya uzazi ambayo tunaonana na wagonjwa kwa wiki mara moja ambapo huwahudumia watu 10 mpaka 12.” Alisema.
  • Mbali na kazi hiyo kinu hicho kinauwezo wa kufua hewa ya Oksijeni ambayo kwa kiwango kikubwa hutumika kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupumua ambapo kwa siku mitungi 400 hufuliwa katika kinu hicho.
KK3-01
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) Dkt. Sarah Urasa akizungumza katika mkutano huo.
  • Dkt. Sarah Urasa aliongeza kuwa: “Hii ni hospitali ya kwanza kuwa na kinu ya kufua hewa ya oksijeni na Nitrogen hapa nchini.
  • Hewa ya Oksijeni pia inatumika kwa wale wagonjwa wanaopewa dawa za usingizi kwaajili ya upasuaji, hewa ya nitrogen inatumika kuhifadhi sampuli kutoka kwa wagonjwa,tiba kwa magonjwa ya ngozi vile vile hutumika kukata matokeo kwenye ngozi au kwenye viungo vya uzazi” alisema.

    Huduma hiyo ambayo imeanza mwaka huu Dkt. Sarah alisema ununuzi wa mitungi ya gesi ya oksijeni pekee ulikuwa ukiwagharimu takribani milioni tatu kwa wiki huku gharama za usafirishaji ikiwa haijajumuishwa hatua ambayo imeokoa gaharama za uendeshaji hospitalini hapo.

  • Dkt.Sarah alieleza kuwa kwa kadiri uzalishaji unavyoongezeka katika kinu hicho wataanza kutumia mfumo wa kuunganisha gesi moja kwa moja hadi katika kitanda cha mgonjwa.
  • “Tumeona uharibifu mkubwa unaotokana namitungi hii ya gesi sakafu yetu imekuwa ikiharibika kutokana na uzito wa mitungi yenyewe kwahiyo mfumo tutakapkuja kuutumia utakuwa bora zaidi tofauti na sasa “alisema.
  • Mafanikio mengine aliyoyataja Dk.Sarah alisema katika utawala wa Rais Dk.John Magufuli wamefanikiwa kuanza kutengeneza maji tiba ‘dripu’ kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa ndani na nje ya hospitali.
  • “Hii inetusaidia kwa kiwango kikubwa hata hospitali zingine zimekuwa zikifika hapa kwaajili ua kujifunza namna ya kutengeneza maji tiba “alisema.
  • Pia alisema KCMC ndio kituo pekee inayotambulika kimaitafa kutoa mafunzo ya magonjwa ya ngozi na zinaa kwa nchi zote za Afrika Mashariki.
  • “Kituo hiki ndio kinachozalisha mafuta ya ngozi kwaajili ya watu wenye ualbino na tayari tumeingia makubaliano na Bohari kuu ya Dawa MSD kwaajili ya kusambaza dawa na tayari tumefikia mikoa 25 kwa kutumia mfumo wetu wa usambazaji na sasa MSD watatuongezea nguvu ili kusambazwa nchi mzima “alisema
  • Kwa upabde wake, Mhandisi KCMC Dustan Kanza alisema mgonjwa mmoja hutumia mtungi mmoja lengo kuepukana na maambukizi.
  • Alisema katika kinu hicho kwa saa 24 inauwezo wa kuzalisha mitungi 400 na mpaka sasa tayari zaidi ya mitungi 600 imezalishwa tangu kuanza kufanya kazi kwa kinu hicho januari mwaka huu.NA ANDREW CHALE, KILIMANJARO.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *