Tanzania MpyA+

WATALII 450 KUTOKA ISRAEL WAKO NCHNI KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII

Watalii zaidi ya 450 kutoka Israel wamewasili nchini mwezi Desemba 2019 kwa ajili ya tembelea vivutio vya kitalii vilivyoko kaskazini mwa Tanzania. Watalii hao wamekuja nchini kwa kutumia ndege binafsi na za kawaida. Kundi la kwanza la watalii 150 liliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 21 Desemba …

Soma zaidi »

UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI UENDE SAMBAMBA NA IDADI KUBWA YA KUWAWASHIA WATEJA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini(REA) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)kuwa kasi ya kuunganisha umeme Vijijini iende sambamba na kasi ya kuwawashia Umeme wateja katika Nyumba zao. Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa …

Soma zaidi »

MINADA YA FORODHA SASA KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imetangaza kusitisha minada ya hadhara ya forodha iliyokuwa ikifanyika hapo awali na badala yake minada hiyo itakuwa ikifanyika kwa njia ya mtandao kupitia Tovuti ya TRA ambayo ni www.tra.go.tz.   Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. …

Soma zaidi »

TUNATAKA MBEGU ZOTE ZIZALISHWE NCHINI – WAZIRI HASUNGA

Serikali imeeleza kuwa imekusudia kuanzisha juhudi wezeshi kuhakikisha kuwa mbegu bora za kilimo zinazalishwa nchini ili kuondokana na wimbi la uagizaji wa mbegu nje ya nchi. Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 22 Disemba 2019 mara baada ya kutembelea kampuni ya Namburi inayojihusisha na uzalishaji wa …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI AFUNGUA KIWANDA CHA NGUZO ZA UMEME – KIGOMA

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefungua kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya, kilichopo katika Mtaa wa Kasanga, Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, mara baada ya ufunguzi wa kiwanda hicho Dkt. Kalemani alieleza kuwa Serikali ilikuwa inapata gharama kubwa kutoa Nguzo katika Mikoa mengine kuzifikisha Mkoani …

Soma zaidi »

TANZANIA YAONGEZA HIFADHI SITA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU

Na Pamela Mollel,Ngorongoro Tanzania imeongeza hifadhi sita (6) kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka hifadhi za Taifa 16 hadi 22 hivi sasa. Hayo yalisemwa na Kamishna Mkuu wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi kama moja ya mafanikio kwenye kongamano la watafiti wa masuala ya uhifadhi, kuelekea …

Soma zaidi »

MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU BANDARI YA KABWE MKOANI RUKWA WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 85

Ujenzi wa mradi wa miundombinu katika Bandari ya Kabwe mkoani Rukwa ambao unagharimu Sh.bilioni 7.498 tayari umekamilika kwa asilimia 85 na mkandarasi wa ujenzi huo ambaye ni Sumry’s Enterprises Ltd anatarajia kuukabidhi mradi huo Aprili mwaka 2020. Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa Mradi wa gati ya Bandari ya Kabwe …

Soma zaidi »