Recent Posts

TAEC YASISITIZA UOMBAJI VIBALI WA NJIA YA MTANDAO

 Wadau na wafanyabiashara nchini wamesisitizwa kupata vibali vya vipimo vya mionzi vinavyotolewa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa njia ya mfumo wa kieletroni kila mara wanapoingiza na kusafirisha bidhaa ndani na nje ya nchi. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Ufundi na Kinga ya Mionzi wa …

Soma zaidi »

MITIHADI YA KIDATO CHA SITA KUFANYIKA KUANZIA JUNI 29, 2020

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka shule zote zenye wanafunzi wa kidato cha sita kuanza maandalizi ya kupokea wanafunzi hao ili waanze masomo Juni 1 2020 kama ilivyoelekezwa. Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati alipoongea na waandishi wa habari ambapo amesema ni vizuri kwa …

Soma zaidi »

TARURA YAENDELEA KUREJESHA MAWASILIANO

Ujenzi wa Kalavati Mstatili (Box culvert), katika barabara ya Bashay- Endaguday- Hydom (inayoelekea Yaedachin wanapopatikana Wahadzabe), ukiwa unaendelea baada ya mawasiliano kukatika kutokana na mvua. Erick Mwanakulya na Geofrey Kazaula – TARURA Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), umeendelea kurejesha mawasiliano katika maeneo mbalimballi yaliyoathiriwa na mvua nchini …

Soma zaidi »

SERIKALI KUWEKEZA SEKTA YA ANGA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellla Manyanya (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye katika kiwanja cha ndege cha Mwanza, mara ya uzinduzi wa safari ya kwanza ya ndege Shirika la Ndege la Ethiopia, ambalo limeanza rasmi jana kuanza kubeba mizigo ya samaki kutokea …

Soma zaidi »

MUDA WA KUKAMILISHA MIRADI HAUJABADILIKA – WAZIRI KALEMANI

Veronica Simba na Zuena Msuya – Dodoma Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini, awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza na kujadiliana maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa nchini kote. Kikao hicho kilichofanyika, Mei 21, 2020 jijini Dodoma kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa …

Soma zaidi »

BODI YA UTALII TANZANIA: TUPO TAYARI KUANZA KUPOKEA WATALII

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema ipo tayari kuanza kupokea watalii wakati wowote kuanzia sasa kufuatia hatua ya Serikali kuruhusu kuendelea kwa shughuli za utalii nchini hatua iliyotokana na kupungua kwa kasi ya mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (CORONA) duniani. Hayo yamesemwa Jijini Dar es Saalam na …

Soma zaidi »

WAKAZI NYAMONGO WALIPWA FIDIA YA BILIONI 33

Bwawa la kuhifadhi Tope Sumu (TFS) katika Mgodi wa Barrick North Mara. Wakazi 1,639 wa Vijiji vya Matongo na Nyabichune katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoa wa Mara wamelipwa fidia ya jumla ya Shilingi Bilioni 33 baada ya kusubiri kwa kipindi cha miaka 10. Fidia hiyo imelipwa Mei 20, 2020 …

Soma zaidi »

WATANZANIA WALIOKUWA WAMEKWAMA ABU DHABI WAREJEA NCHINI

Watanzania 119 waliokuwa wamekwama Abu Dhabi (Dubai) wamerejea Tanzania na kutoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na jitihada za kuwarejesha nyumbani. Watanzania 119 waliokuwa wamekwama Abu Dhabi (Dubai) baada ya mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona na kusababisha mashirika mbalimbali ya ndege kufunga safari …

Soma zaidi »