WAKAZI NYAMONGO WALIPWA FIDIA YA BILIONI 33

Bwawa la kuhifadhi Tope Sumu (TFS) katika Mgodi wa Barrick North Mara.

Wakazi 1,639 wa Vijiji vya Matongo na Nyabichune katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoa wa Mara wamelipwa fidia ya jumla ya Shilingi Bilioni 33 baada ya kusubiri kwa kipindi cha miaka 10.

Fidia hiyo imelipwa Mei 20, 2020 na Mgodi wa  Barrick North Mara  ikiwa  Utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli aliyoyatoa wakati wa ziara yake Mkoani humo ambapo alitaka suala hilo ikiwemo la uchafuzi wa mazingira yamalizwe haraka.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa utoaji fidia  na Ugawaji wa Cheki kwa Wakazi hao waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ajili ya uendelezaji wa shughuli za mgodi huo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishi wote wenye haki ya kulipwa fidia hiyo kuwa watalipwa fedha zao.

Aidha, ametoa pongeza kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kueleza kuwa Wizara hiyo ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha inamaliza mgogoro wa fidia uliokuwepo baina ya wananchi na mgodi huo.

Pia, amempongeza Mthamini Mkuu wa Serikali kwa kazi ya uthamini iliyofanyika hatimaye kuwezesha wananchi wanaopaswa kulipwa  fidia zao wanalipwa na kuongeza, ” maisha ya kutegesha yamekwisha, Serikali haitakubali kushuhudia watengeneza migogoro wakitengeneza migogoro hapa”.

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.