WATANZANIA WALIOKUWA WAMEKWAMA ABU DHABI WAREJEA NCHINI

Watanzania 119 waliokuwa wamekwama Abu Dhabi (Dubai) wamerejea Tanzania na kutoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na jitihada za kuwarejesha nyumbani.

Watanzania 119 waliokuwa wamekwama Abu Dhabi (Dubai) baada ya mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona na kusababisha mashirika mbalimbali ya ndege kufunga safari zake wamewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nane mchana kwa ndege ya shirika la ndege la Fly Dubai.


Wakizungumza wakati na  baada ya kumaliza taratibu zote za uhamiaji baadhi ya Watanzania hao ambao wengine walikuwa na watoto wadogo wamesema Maisha ya kufungiwa ndani kwa takribani miezi mitatu si rahisi hata kidogo jambo lililosababisha ugumu wa Maisha baada ya wengine akiba zao kumalizi,Bi Christina Magige,mtanzania aliyerejea

Ad

Kwa upande wake Bw Yahaya Abdala amesema Maisha ugenini hayakuwa rahisi baada ya kukwama kwa kuwa walishindwa kurejea Tanzania kwa mara ya kwanza kutokana na idadi ya wasafiri kuwa ndogo lakini kwa jitihada za Serikali baadae kibali cha safari kilipatikana na hatimae wamerejea Tanzania,Bw. yahaya Abdalah,mtanzania aliyerejea

Hii ni mara ya pili kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuratibu na kufanikisha safari ya

watanzania kurejea nyumbani baada ya kukwama ughaibuni kutokana na changamoto ya uwepo wa Virusi vya Corona na kusababisha mashirika mengi ya ndege kusitisha safari zake ambapo awali takribani watanzania 246 walirejeshwa na serikali wakitokea India.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *