Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashini za kutoa tiba ya saratani macho kwa watoto bila kuyaondoa zenye thamani ya shilingi milioni 170 kutoka Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam. Msaada huu utawanufaisha watoto wengi wanaofikishwa hapa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma ya saratani ya …
Soma zaidi »MADAKTARI NA WAUGUZI KUPATIWA FURSA ZAIDI YA MAFUNZO KATIKA FANI YA UBONGO NA MISHIPA NCHINI CHINA
WAGONJWA 15 KUPATA MATIBABU YA KUZIBUA MISHIPA YA DAMU YA MOYO
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao wa Hospitali ya Meditrina ya nchini India wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa siku tatu ya kuzibua mishipa ya damu ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa (Chronic Total Occlusion) na hivyo kushindwa kupitisha damu vizuri. …
Soma zaidi »NAIBU WAZIRI WA AFYA AZINDUA MAABARA YA KISASA YA MAFUNZO
Katika kuadhimisha Siku ya Afya Duniani, Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile amezindua maabara ya kisasa itakayotoa mafunzo kwa vitendo kwa wataalamu wa huduma za usingizi na dharura, MUHAS
Soma zaidi »TAASISI YA MIFUPA (MOI) NA BMVSS YA INDIA KUTOA MIGUU BANDIA 600 BURE
Taasisi ya Mifupa MOI kwa kushirikiana na Taasisi ya BMVSS ya India wataendesha zoezi la kutoa miguu bandia 600 BURE. taarifa zinaksema wote wenye uhitaji wafike MOI ndani ya mwezi April 2019 kwa vipimo na miguu hiyo itatolewa mwezi May 2019
Soma zaidi »UPASUAJI SARATANI YA MATITI SASA UNAFANYIKA BILA KULIONDOA
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na kampuni ya dawa ya Roche ya nchini Kenya imeandaa mkutano wa kisayansi wa kuwajengea uwezo wataalam wa Radiolojia, Pathiolojia, Upasuaji, tiba ya mionzi na dawa kufanya upasuaji wa saratani ya matiti kwa kutoa uvimbe bila kuondoa titi lote kwa wagonjwa wenye dalili za …
Soma zaidi »HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MLOGANZILA WATOA HUDUMA YA UPIMAJI USIKIVU BILA MALIPO
Wingi wa watu waliojitokeza kupima usikivu wao umeonyesha ni jinsi gani wananchi wanajali afya zao, huku wakipewa sababu zinazosababisha baadhi ya watu kupoteza uwezo wa kusikia na jinsi ya kuzuia upotevu wa kusikia. Upimaji wa usikivu bila malipo umeanza Machi 2, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ambapo kauli mbiu …
Soma zaidi »MOI WAENDESHA KAMBI YA UPANDIKIZAJI WA NYONGA BANDIA NA UPASUAJI WA MGONGO
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikianana hospitali ya Zydus ya nchini India kuanzia leo tarehe 14/02/2019 mpaka tarehe 16/02/2019 zitaendesha kambi maalum ya upandikizaji wa nyonga bandia na upasuaji wa Mgongo kwa njia ya kisasa. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema Katika kambi hii Madaktari bingwa wa …
Soma zaidi »MLOGANZILA IMEBORESHA HUDUMA KWA WANANCHI NA ITAENDELEA KUBORESHA ZAIDI – PROF.MAJINGE
Bodi ya Wadhamini, Hospitali ya Taifa Muhimbili imeupongeza Uongozi wa kwa kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika Hospitali ya Mloganzila. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Prof. Charles Majinge katika kikao cha kawaida cha Bodi hiyo kilichofanyika Hospitali ya Mloganzila ambapo Menejimenti iliwasilisha taarifa ya utendaji …
Soma zaidi »MUHIMBILI YAFANYA UCHUNGUZI WA AWALI WA KUANGALIA UVIMBE KWENYE MATITI BILA KUFANYA UPASUAJI
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) leo imetoa huduma ya uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu amesema katika zoezi hilo endapo mgonjwa …
Soma zaidi »