Wananchi katika Kijiji cha Igando, wilayani Chato, mkoa wa Geita, wameanza kupata huduma ya umeme kupitia mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu (REAIII) unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ndiye aliyewasha rasmi umeme katika …
Soma zaidi »WACHIMBAJI WADOGO KUFIKISHIWA UMEME KWENYE MASHIMO YAO
Wachimbaji wadogo mkoani Geita wanatarajiwa kufikishiwa Umeme katika mashimo yao ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa ufanisi mkubwa. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita. Alisema kuwa Serikali inatambua mchango …
Soma zaidi »TANESCO INATEKELEZA MIRADI MIKUBWA 22 KWA WAKATI MMOJA
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wataondokana na tatizo la umeme baada ya transfoma yenye uwezo wa MVA 300 sawa na Mw 240 kuwasili. Transfoma hiyo itakiongezea uwezo kituo cha Ubungo kutoka MVA 300 hadi 600 sawa na MW 480. Kazi hii itakamilika Mwezi Mei …
Soma zaidi »UJENZI WA MRADI WA UMEME RUFUJI KUANZA RASMI MWENZI JUNI
Imeelezwa kuwa ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji utakaozalisha megawati 2115 unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 mwezi Juni mwaka huu. Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani katika eneo utakapotekelezwa mradi huo wilayani Rufiji mkoani Pwani mara baada ya kukagua kazi za ujenzi wa miundombinu wezeshi …
Soma zaidi »UJENZI WA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA WASHIKA KASI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua amewaasa wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa za kazi za ujenzi zinazoendelea katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma. Katibu Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dodoma baada ya kukagua kazi ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati ambapo …
Soma zaidi »WAZIRI KALEMANI AWATAKA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME KUELEZA MIPANGO KAZI YAO KWA VIONGOZI
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchini kote, kuwasilisha mipango-kazi yao kwa viongozi na wawakilishi wa wananchi wa maeneo wanakofanyia kazi ili waweze kuielewa hivyo kusimamia utekelezaji wake. Alitoa maagizo hayo jana, Desemba 30, 2018 wilayani Ukerewe akiwa katika ziara ya kazi kukagua …
Soma zaidi »MKANDARASI JENGO LA WIZARA YA NISHATI ATAKIWA KUKAMILISHA KAZI YA UJENZI KWA WAKATI
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemtaka mkandarasi anayetekeleza kazi ya ujenzi wa Jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa. Akizungumza katika eneo la Ihumwa WaziriKalemani amesema kuwa, ili kufanikisha utekelezaji wa kazi hiyo kwa wakati …
Soma zaidi »WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA IPARAMASA
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewasha umeme katika Kijiji cha Iparamasa, Wilaya ya Chato mkoani Geita, tukio lililoibua shangwe na nderemo kwa wananchi wa eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika jana, Desemba 21, 2018 kijijini hapo, wakati Waziri akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini …
Soma zaidi »Nishati ya umeme itasaidia ukuaji wa uchumi wa viwanda – Naibu Waziri Sima
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amezitaka nchi zilizoendelea kutimiza wajibu wao wa kutoa michango ya fedha na kuwezesha upatikanaji wa teknolojia za kisasa kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabianchi kwa mujibu wa …
Soma zaidi »Wakandarasi wa Umeme Acheni Visingizio – Waziri wa Nishati
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza Mradi ya kusambaza umeme vijijini (REA III) kuacha visingizio vinavyochelewesha mradi huo kukamilika kwa wakati. Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo wakati akizungumza wakandarasi wanaotekeleza mradi huo katika mikoa ya Mwanza na Manyara juu ya maendeleo ya utekelezaji REA III, mzunguko wa kwanza …
Soma zaidi »