Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita.

WANANCHI WA IGANDO WAANZA KUPATA HUDUMA YA UMEME

  • Wananchi katika Kijiji cha Igando, wilayani Chato, mkoa wa Geita, wameanza kupata huduma ya umeme kupitia mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu (REAIII) unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
  • Waziri wa Nishati, Dkt  Medard   Kalemani ndiye aliyewasha rasmi umeme  katika Kijiji hicho,ambapo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Chato,  Mhandisi Mtemi Semeon na viongozi wengine kutoka Wilaya hiyo, Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  • Aidha, kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Igando, Dkt Kalemani alifika katika Kijiji cha Imwelu kilichopo Kata ya Buseresere wilayani humo ili kukagua kazi ya upelekaji wa miundombinu ya umeme katika Kijiji hicho.
  • Akiwa kijijini hapo, Dkt Kalemani aliwaagiza REA, TANESCO pamoja na mkandarasi aliyepewa kazi ya kusambaza umeme kijijini hapo, kuhakikisha kuwa, ifikapo tarehe 28 mwezi huu, kijiji hicho kiwe kimeshawashiwa umeme.
  • Kwa nyakati tofauti akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo, alisisitiza kuwa, bei ya uunganishaji umeme katika vijiji vyote nchini ni shilingi 27,000, tu, hivyo wananchi wa vijijini wasitozwe zaidi ya kiasi hicho.
  • Aidha, amewataka wananchi hao kutumia umeme huo pia kwa shughuli za maendeleo ambazo zitawaongezea kipato na kukuza uchumi katika maeneo mbalimbali nchini.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *