Maktaba Kiungo: NAIBU WAZIRI WA NISHATI

TUMIENI UMEME KUANZISHA MIRADI YA MAENDELEO – DKT. KALEMANI

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaasa wananchi wa Kitongoji cha Mwamagili, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kutumia umeme aliowawashia rasmi jana, Juni 30, 2019 kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.   Akizungumza na wananchi hao muda mfupi kabla ya kuwasha umeme katika nyumba ya mkazi wa kitongoji hicho, Kashonele …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI ATIMIZA AHADI YAKE KUWAWASHIA UMEME WANANCHI WA MWAKITOLYO

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametimiza ahadi yake aliyoitoa mwanzoni mwa mwezi huu (Juni) kwa wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, kuwa umeme utawashwa katika eneo lao kabla ya Julai, 2019. Dkt. Kalemani alitimiza ahadi hiyo jana, Juni 29, 2019 akiwa katika ziara ya kazi mkoani Shinyanga, …

Soma zaidi »

TANESCO YATENGA TSHS. BILIONI 400 KUPELEKA UMEME KWENYE MAENEO YALIYOPITIWA NA MIUNDOMBINU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetenga kiasi cha shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kazi ya kusambaza umeme kwenye maeneo takribani 754 yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme lakini hayana umeme. Hayo yalisemwa tarehe 24 Juni, 2019 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati wa Majumuisho ya Semina …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI MGALU AWASHA UMEME NJOPEKA MKOANI PWANI

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, jana Juni 23, 2019 alikiwashia rasmi umeme kijiji cha Njopeka kilichopo wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Aliwasha umeme huo kwenye Duka la Abdul Abdulrahman, ikiwa ni ishara ya kukiwashia kijiji kizima. Kabla ya tukio la kuwasha umeme, Naibu Waziri alizungumza na wananchi wa eneo …

Soma zaidi »

SERIKALI KUFANYA UPEMBUZI YAKINUFU KWA AJILI YA UPANUZI WA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE(JKCI)

Tanzania imetia saini Mkataba wa kupatiwa fedha za Msaada wa Shilingi Bilioni 60 za kitanzania kutoka Serikali ya Watu wa China bila ya masharti yeyote ambapo Serikali ya Tanzania itaamua matumizi yake katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake. Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na …

Soma zaidi »

MAMENEJA TANESCO TUTAWAPIMA KWA KAZI ZENU – NAIBU WAZIRI MGALU

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa wito kwa Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Ngazi ya Mkoa na Wilaya nchi nzima, kufanya kazi kwa bidii kwani ndicho kigezo kitakachotumiwa kuwapima iwapo wanafaa kuendelea kushikilia nyadhifa hizo. Alitoa wito huo Juni 22, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI MGALU AZURU KONDOA KUJIRIDHISHA NA ELFU 27 YA UMEME VIJIJINI

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya ziara wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa agizo la Serikali kuhusu kuwezesha wananchi wote wanaopitiwa na miradi ya umeme vijijini (REA), kulipia shilingi 27,000 tu bila kujali ni vijijini au katika Halmashauri za Wilaya. Alifanya ziara hiyo jana, …

Soma zaidi »

MAMENEJA WA TANESCO WATAKIWA KUTEMBELEA VIWANDA KWENYE MAENEO YAO

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ametoa Siku Saba kwa Mameneja wa TANESCO kote nchini kutembelea viwanda kwenye maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha kuwa viwanda hivyo vinapata umeme wa uhakika kwa ajili ya uzalishaji na kufanya utatuzi endapo kutakuwa na changamoto ya kutokuwepo kwa umeme kwenye maeneo hayo. Aliyasema …

Soma zaidi »

WIZARA YA NISHATI, TANESCO NA REA WAJADILI MIPANGO YA USAMBAZAJI UMEME KWA MWAKA 2019/20

Ili kuhakikisha kuwa kazi ya usambazaji umeme mijini na vijijini inafanyika kwa kasi na ufanisi katika mwaka wa fedha 2019/20, viongozi wa Wizara ya Nishati wakiongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wamefanya Mkutano wa siku moja na watendaji wa TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kujadili …

Soma zaidi »

MKANDARASI WA MRADI WA UMEME WA RUFUJI (MW 2115) KUANZA UJENZI RASMI LEO

Imeelezwa kuwa, Mkandarasi wa mradi wa umeme wa Rufiji, kampuni ya JV Arab Contractors na Elsewedy Electric anaanza rasmi kazi za ujenzi wa mradi huo leo tarehe 15/6/2019. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani baada ya ziara ya kukagua kazi za maandalizi ya awali ya ujenzi wa …

Soma zaidi »