Maktaba Kiungo: NAIBU WAZIRI WA NISHATI

MAWAZIRI WA NISHATI WA AFRIKA MASHARIKI WAAHIRISHA MKUTANO WAO

Mawaziri wenye dhamana na sekta ya nishati kutoka nchi sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameahirisha Mkutano wao uliopangwa kufanyika Arusha, Juni 7 mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa EAC anayeshughulikia Sekta ya Uzalishaji, Jean Baptiste Havugimana, ilieleza kuwa Mkutano huo utafanyika siku nyingine katika tarehe itakayobainishwa na …

Soma zaidi »

WANANCHI CHIBOLI KUFURAHIA SIKUKUU YA EID EL-FITR NA UMEME

Wananchi katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, Jimbo la Mtera, watasherehekea sikukuu ya Eid El-fitr wakiwa na umeme kwa mara ya kwanza, baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kuwasha umeme katika Kijiji hicho. Akiwa ameambatana Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga, …

Soma zaidi »

MKUTANO WA NISHATI KWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAANZA ARUSHA

Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki, umeanza  Juni 3, 2019 jijini Arusha. Akifungua Mkutano huo katika siku ya kwanza ambao unahusisha ngazi ya wataalamu wa sekta husika; Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TPDC

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), yatakayofanyika kesho tarehe 31 Mei, 2019 jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba, tarehe 30/5/2019, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME SAMUNGE NA DIGODIGO WILAYANI NGORONGORO

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasha umeme katika Vijiji vya Samunge na Digodigo vilivyopo wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kumtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini wilayani humo kuongeza kasi zaidi. Akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme wilayani humo, Waziri Kalemani …

Soma zaidi »

SERIKALI YAJIPANGA KUUNGANISHA GESI ASILIA MAJUMBANI NCHI NZIMA

Serikali imesema Mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ni endelevu na utafanyika katika mikoa yote nchi nzima awamu kwa awamu. Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, alibainisha hayo jana, Mei 25, 2019 jijini Dodoma katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ambayo ililenga kuwajengea …

Soma zaidi »

MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI WAZINDULIWA

Serikali imezindua Mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa Vijiji, Wilaya na Mikoa itakayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ikiwa ni hatua nyingine katika utekelezaji wa mradi huo. Mpango huo umezinduliwa katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora tarehe …

Soma zaidi »

WABUNGE WA LINDI NA MTWARA WATOA HOJA KATIKA WARSHA KUHUSU MRADI WA GESI ASILIA ILIYOSINDIKWA (LNG)

Hoja  1. Fidia kwa wananchi Ufafanuzi wa Serikali Fidia ni haki, ni stahiki na ni jambo la kisheria. Kama Serikali, hatuwezi kulipindisha. Tunachofanya ni kujihakikishia kwamba watakaofidiwa ni wale tu wanaostahili kweli. Kutokana na umuhimu wa jambo hili, lazima lifanyike kwa umakini sana. Ipo hatari ya kulipa haraka-haraka, kisha wakajitokeza …

Soma zaidi »

KIPAUMBELE CHA WIZARA NI KUPELEKA NISHATI KWA WANANCHI

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaeleza watumishi wa Wizara ya Nishati kuwa kipaumbele cha Wizara ni kupeleka nishati kwa wananchi ikiwamo ya Umeme na Gesi hivyo amewaasa kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa weledi. Dkt. Kalemani alitoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara …

Soma zaidi »

SERIKALI KUMALIZA TATIZO LA KUKATIKA UMEME, KOROGWE

Serikali imesema changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara wanayoipata wananchi wa Korogwe inafanyiwa kazi na  itaisha ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja kuanzia sasa, hivyo wawe wenye subirá na waondoe hofu. Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani aliyasema hayo kwa nyakati tofauti jana, Mei 19, 2019 akiwa katika ziara …

Soma zaidi »