Maktaba Kiungo: Tanzania Mpya

MCHEZAJI WA ZAMANI TIMU YA TAIFA PETER TINO AKABIDHIWA Tsh.MILLIONI 5 ALIZOPEWA NA RAIS MAGUFULI

Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino amekabidhiwa shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambayo ilifuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya …

Soma zaidi »

WAZIRI KAMWELWE AWATAKA WATUMISHI SEKTA YA UJENZI KUONGEZA UBUNIFU

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kuongeza ubunifu na bidii katika kazi wanazozifanya ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani. Mhandisi Kamwelwe, amesema kuanzia sasa wafanyakazi wa sekta hiyo wawekewe mkakati utakaowapa …

Soma zaidi »

KIGOMA KUPATA UMEME WA GRIDI APRILI MWAKANI

Imeelezwa kuwa, Mkoa wa Kigoma utaanza kupata umeme wa Gridi kuanzia mwezi Aprili mwakani hali itakayopelekea Mkoa huo kupata umeme wa uhakika na Serikali kuokoa fedha zinazotumika kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme kwa sasa. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani katika wakati wa ziara yake …

Soma zaidi »

TANZANIA YAPATA HESHIMA KWENYE MKUTANO WA SOUTH – SOUTH COOPERATIONS, BUENOS AIRES, ARGENTINA.

Tanzania imesifiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Uhusiano wa Nchi za Kusini (UNOSSC) , Umoja wa nchi Afrika, Karibian na Pasifiki (ACP) pamoja na nchi mbalimbali kwa namna ambavyo inapambana kulinda rasimali zake za asili na kudhibiti utoroshaji haramu wa fedha toka Afrika kwenda kwenye nchi zilizoendelea. Akiwasilisha …

Soma zaidi »

WAFANYABIASHARA TANZANIA SASA WANAWEZA KUTAFUTA MASOKO NCHINI CHINA KUPTIA E-COMMERCE

Makampuni ya Tanzania yametafutiwa fursa ya kutafuta masoko ya bidhaa zake nchini China kwa njia ya mtandao, hayo yameelezwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya China-Africa E-Commerce ndugu Zhigang Hou alipokutana na Balozi wa Tanzania Nchini China Mbelwa Kairuki jijini Chengdu katika jimbo la Sichuan. Makampuni ya Tanzania yanayohitaji kuuza bidhaa …

Soma zaidi »

TANZANIA, UGANDA ZAJADILIANA ULINZI BOMBA LA MAFUTA

Ikiwa ni muendelezo wa majadiliano mbalimbali kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania (EACOP), Kamati za Ulinzi na Usalama za mradi kutoka  nchi hizo zimekutana jijini Kampala kwa lengo kujadili masuala ya usalama ya mradi huo. Kikao kati ya pande hizo mbili kilianza tarehe 18/3/2019 na …

Soma zaidi »

VIJANA WAANZA KUITIKIA WITO WA KUCHAPA KAZI KIZALENDO

Vijana wa kijiji cha Chihwindi kata ya Mtumachi, Newala mkoani Mtwara wamefyeka uwanja  wa kijiji hicho kwaajili ya ujenzi wa kiwanja hicho cha timu ya kijiji maarufu kwa jina la POCHI NENE. Akizungumzia tukio hilo Ndugu Musa Shaibu, amesema kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kuhamasisha vijana kujitolea kufanya kazi …

Soma zaidi »

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), unaoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa KM 300 na  kusisitiza kuwa Bunge litaendelea kupitisha fedha za mradi huo hadi utakapokamilika kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Mwenyekiti wa Kamati …

Soma zaidi »