TANZANIA, UGANDA ZAJADILIANA ULINZI BOMBA LA MAFUTA

  • Ikiwa ni muendelezo wa majadiliano mbalimbali kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania (EACOP), Kamati za Ulinzi na Usalama za mradi kutoka  nchi hizo zimekutana jijini Kampala kwa lengo kujadili masuala ya usalama ya mradi huo.
WATAALAM
Wataalam kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha majadiliano kilichohusu masuala ya usalama katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
  • Kikao kati ya pande hizo mbili kilianza tarehe 18/3/2019 na kuhitimishwa tarehe 20 mwezi huu  na Wawakilishi wa Wakuu  wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa nchi hizo mbili ambapo  kuliandaliwa Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi wa Bomba la Mafuta.
  • Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi huo yanatarajiwa kusainiwa katika vikao vijavyo vya ngazi ya Mawaziri wa nchi husika.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KALEMANI AFUNGUA KIWANDA CHA NGUZO ZA UMEME – KIGOMA

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefungua kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya, kilichopo katika Mtaa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *