MCHEZAJI WA ZAMANI TIMU YA TAIFA PETER TINO AKABIDHIWA Tsh.MILLIONI 5 ALIZOPEWA NA RAIS MAGUFULI

Screen Shot 2019-03-25 at 16.54.13

  • Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino amekabidhiwa shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambayo ilifuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON).
  • Peter Tino ndiye aliyefunga goli lililoiwezesha Tanzania kuingia robo fainali na tangu mwaka 1980 Tanzania haikufanikiwa kuingia hatua hiyo mpaka mwaka 2019 ikiwa ni miaka 39 imepita.
  • Peter Tino amealikwa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Machi, 2019 wakati Mhe. Rais Magufuli alipokutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambao jana waliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) na kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadaye mwezi Juni 2019 huko Misri.
  • Pamoja na kupatiwa shilingi Milioni 5, Peter Tino ameunganishwa katika zawadi ya kupatiwa kiwanja Jijini Dodoma kwa kila mchezaji wa Taifa Stars iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli ambapo naye atapatiwa kiwanja cha kujenga nyumba.
  • Fedha za Peter Tino zimewekwa katika akaunti yake ya Benki ya CRDB na kukabidhiwa kadi yenye taarifa zake za benki (ATM).

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.