Maktaba Kiungo: WIZARA YA MADINI

WIZARA ITAENEDLEA KUANZISHA MASOKO YA MADINI – WAZIRI BITEKO

Wizara ya Madini itaendelea kusimamia Uanzishwaji wa Masoko ya Madini katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiendelea kufanya marekebisho ya Kanuni za Uanzishwaji wa masoko hayo. Waziri wa Madini Doto Biteko ameyasema hayo Machi 31, 2019 wakati akifunga Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na wizara kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu …

Soma zaidi »

PROF PALAMAGAMBA AKUTANA NA BARONESS LYNDA CHALKER

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesema mabadiliko yote ya sheria yaliyofanyika hivi karibuni katika sekta za madini,maliasili na uwekezaji yana lengo la kuweka mazingira bora zaidi yatakayoleta tija kwa Taifa na wawekezaji kutokana  na sheria mpya kuondoa utaifishaji (nationalization) na upokonyaji …

Soma zaidi »

WAZIRI BITEKO AZINDUA BODI YA GST

Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), imetakiwa kuiwezesha taasisi hiyo kurahisisha maisha ya Wachimbaji Wadogo, wa Kati na Wakubwa kwa kuhakikisha wanapata taarifa za tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizundua Bodi ya GST na kueleza kuwa, …

Soma zaidi »

LIVE CATCH UP: WAZIRI PROF. KABUDI AKIZUNGUMZIA UJUMBE ULIOFIKA NCHINI KUTOKA QATAR NA NORWAY

Aelezea ujio wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Qatar aliyefika nchini siku Jumatano tarehe 20 Machi, 2019 na kuondoka Alhamisi tarehe 21 Machi, 2019. Qatar kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye uchimbaji na uvunaji wa gesi pamoja na uwekezaji katika uwekezaji wa hoteli …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA SOKO LA DHAHABU MJINI GEITA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa atakayekamatwa anatorosha madini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha. Pia amewataka viongozi na watendaji wote wa Serikali wasimamie kwa weledi, uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo kuhusu sekta ya madini kwa lengo la …

Soma zaidi »

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAPONGEZA MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO – SONGEA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Mwenyekiti, Mariamu Ditopile Mzuzuri, imeipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi wa umeme wa Makambako- Songea (kV 220) ambao umewezesha Mikoa ya Ruvuma na Njombe kupata umeme wa uhakika kutoka Gridi ya Taifa. Kamati hiyo, imetoa pongezi hizo wilayani Songea, Mkoa …

Soma zaidi »

WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini. Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya …

Soma zaidi »

MAKAMU WA RAIS AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kuwainua Wanawake, Vijana na Walemavu ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa katika makundi hayo ndani ya kipindi cha 2017 – 2018. Makamu …

Soma zaidi »

WACHIMBAJI WADOGO WILAYANI MBOGWE KUPATA UMEME NDANI YA SIKU KUMI

Wachimbaji wadogo katika machimbo ya Nyakafuru yaliyo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe wameonesha kufurahishwa na ahadi ya Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ya kufikisha umeme katika machimbo hayo ndani ya siku kumi. Ahadi hiyo aliitoa jana mara baada ya kufanya ziara ya kikazi wilayani Mbogwe mkoani Geita ambapo …

Soma zaidi »