Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba wilayani Kaliua, Tabora.

MAKAMU WA RAIS AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA

  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kuwainua Wanawake, Vijana na Walemavu ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa katika makundi hayo ndani ya kipindi cha 2017 – 2018.
JENGO LA UPASUAJI
Picha ya Jengo la Upasuaji lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya halmashauri na michango ambalo limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo wilayani Kaliua, Tabora.
  • Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Kolimba, Kaliua moani Tabora.
  • Aidha katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameridhia kuondolewa mara moja kwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kaliua Mhandisi Fikiri Samadi baada ya kushindwa kutekeleza mradi wa maji wa shilingi bilioni 1.5.
TABORA-4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa zaidi ya pikipiki 15 kwa vijana wa boda boda ikiwa ni mkopo kutoka Halmashauri ya Kaliua, Tabora.
  • “Ziara hizi ni ziara za kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na serikali imekuwa mstari wa mbele kuweka pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo hivyo yeyote atakayekwamisha atachukuliwa hatua mara moja”alisema Makamu wa Rais.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo la Urambo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Margaret Sitta mara baada ya kuhutubia katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Usoke Mlimani.
  • Makamu wa Rais amesema wilaya ya Kaliua ni mfano wa kuigwa kwa kujenga jingo la upasuaji pamoja na wodi ya wazazi yenye uwezo wa kuchukua vitanda 24 katika kituo cha afya Kaliua kwa mapato yao ya ndani pamoja na michango kutoka chama cha msingi Nsungwa ambapo mpaka kukamilika wametumia shilingi 159,703,199.98.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni 250 kwa vikundi 61 vya ujasiriamali ukiwa ni mkopo kutoka Halmashauri ya Kaliua, Tabora.
  • Kwa upande mwingine Naibu Waziri TAMISEMI amesema vikundi vinavyopewa mikopo na Halmashauri lazima virejeshe mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia watu wengine akizungumzia kwa wilaya ya Kaliua peke yake ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa mpaka sasa zimerudishwa milioni 89 tu.
WAZIRI WA MADINI
Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora
  • Akizungumzia suala la uchaguzi katika kata 3 za Igombe Mkuluu, Mirambo na Kanindo zilizopo katika jimbo la Ulyankulu, Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Waitara amesema lazima usalama wa Taifa uzingatiwe na upewe kipaumbeke kwani kwenye maeneo hayo kuna waliopewa uraia na kuna wakimbizi hivyo Serikali itakapojiridhisha wanaweza shiriki katika uchaguzi ujao.
NAIBU WAZIRI
Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji Juma Aweso akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora katika ziara ya Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan
WANANCHI
Sehemu ya wakazi wa Usoke Mlimani walioihudhuria mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Urambo mkoani Tabora.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

WANANCHI JIMBO LA MTERA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJISAFI NA SALAMA

Serikali  imepongezwa kwa kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma ya majisafi na salama baada ya miaka …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *