IRINGA: “Unganishiwa umeme kwa bei nafuu ya mradi wa REA ya shilingi elfu 27 tu” Mhe.Kalemani

YALIYOJIRI KWENYE KIPINDI CHA TUNATEKELEZA KILICHOMUHUSISHA WAZIRI WA NISHATI, DKT. MEDARD KALEMANI 13/09/2018.

#Mradi wa Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme uliopo Makambako, umekamilika

Ad

 

#Utekelezaji wa mradi huu ulianza Septemba 2016, pia ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi

#Sehemu ya kwanza ya mradi huu imehusisha ujenzi wa vituo vitatu vya kufua umeme mkubwa wa kilowatts 220 vilivyojengwa Makambako, Madaba na Songea

 

#Sehemu ya pili ya mradi imehusisha ujenzi wa miundombinu ya kusafirishia umeme unaofuliwa katika vituo hivyo vitatu

makambako picha tatu.JPG

#Sehemu ya tatu ya mradi ni kusambaza umeme katika vijiji 122 vya mikoa miwili ya Njombe na Ruvuma

#Mradi wa Umeme Makambako-Songea utaunganisha wateja wa awali wapatao 22,700 na kadri unavyoendelea wananchi wengi zaidi wataendelea kuunganishwa

#Mradi wa Umeme wa Makambako-Songea umegharimu shilingi bilioni 216 ambazo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sweden

#Ni matarajio yetu kuwa mradi huu utafunguliwa rasmi mwisho wa mwezi huu wa Septemba

#Ifikapo Septemba 26 mwaka huu tutawasha mitambo na wananchi wataanza kutumia umeme kutoka kwenye mradi huu wa Makambako-Songea

 

 

 

#Mradi huu utakuwa na manufaa makubwa ikiwemo wananchi kuunganishiwa umeme kwa bei nafuu ya mradi wa REA ya shilingi elfu 27

#Tukiwasha mitambo ya mradi huu tutazima rasmi mitambo ya umeme iliyokuwa inatumia mafuta mazito iliyoko Madaba, Ludewa, Mbinga, Namtumbo na Songea Mjini

#Mitambo ya umeme inayotumia mafuta mazito ilikuwa inagharimu shilingi bilioni 1.9 kwa mwaka

#Natoa wito kwa wananchi watumie umeme huu mkubwa kwa ajili ya kujenga uchumi wa viwanda

#Sasahivi tuna jumla ya Megawatts 1568 kwenye gridi ya taifa

#Mradi wa Umeme wa Mto Rufiji (Stigler’s Gorge) utajengwa kwa miaka mitatu na ukikamilika utazalisha Megawatts 2100 zitakazoingia kwenye gridi ya taifa

#Mradi wa Umeme wa Rusumo unatekelezwa katika nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi na utazalisha megawatts 80 ambapo kila nchi itapata takriban megawatts 27

#Mradi wa Rusumo utasambaza umeme katika vijiji 58 kwenye mikoa ya Kigoma na Kagera

#Mradi wa REA III unatarajiwa kuunganisha umeme kwenye vijiji 5100 nchini ambapo kuanzia Julai hadi Septemba 2018 tayari vijiji 818 vimeshaunganishwa

Naibu-Waziri

#Tunatarajia ifikapo Juni 2021 vijiji vyote 12,268 vya Tanzania vitakuwa vimeunganishiwa umeme

#Mradi wa kuzalisha megawatts 600 za umeme wa makaa ya mawe utaanza Julai 2019

Upepo umeme.jpg

#Kuanzia tarehe 15 Septemba 2018 tumetangaza kuwa wawekezaji wenye nia na uwezo wa kuzalisha umeme wa upepo na jua waje kuanza uzalishaji

 

#Miaka miwili ijayo tutaanza kuzalisha megawatts 30 za umeme wa jotoardhi

KinyereziI1.jpg

#Mradi wa Kinyerezi umekamilika kwa asilimia 100, hadi sasa tumeingiza megawatts 218 kwenye grid ya taifa na kufikia mwisho wa mwezi huu megawatts zote zitakuwa zimeingia

Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Ad

Unaweza kuangalia pia

USHAWISHI WA TANZANIA DUNIANI UTATEGEMEA NA UBORA WA SERA YA MAMBO YA NJE INAYOREKEBISHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe.  Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya …