WAZIRI JENISTA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI CHA MKULAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Mkulazi (Mbigili) Mkoani  Morogoro kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kuelekea katika hatua ya kuanza uzalishaji.
KAIMU MKURUGENZI WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi Bw. Gerald Sondo akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) eneo la shamba walilopanda hekta 860 za miwa ambayo imekwa bila kutegemea umwagiliaji.
Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Mhagama amewataka watendaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha wanatumia mradi huo kwa manufaa ya Taifa na kuwasisitizia wafanye kazi kwa weledi ili  kuendeleza kiwanda hicho wakizingatia uadilifu katika utendaji kazi wao.
“Lazima kila mmoja wenu atekeleze majukumu yake kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Serikali ili azma ya kuanzishwa kwa kiwanda hiki itimie, kwa kuwa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt John Magufuli ni kuhakikisha kuwa inajenga uchumi wa viwanda ambao ni jumuishi na unalenga kuwanufaisha wananchi wote na manufaa ya kiwanda hiki ni kwa wanachama”. Alisisitiza Mhe Mhagama
WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na watendaji wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kuhakikisha wanatumia mradi huu kuleta manufaa yanayotarajiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio  ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Waziri  Mhagama na kumhakikishia  kuwa watashirikiana na Bodi ya Wadhamini ya Shirika hilo kusimamia kwa uadilifu mkubwa mradi huo.
Pia amesisistiza kuwa wataendelea kufanya juhudi kubwa katika kutekeleza mipango yote itakayowezesha kuanza mapema iwezekanavyo kwa uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho.
Screen Shot 2018-10-02 at 12.40.13 PM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya watendaji alipowasili katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi (Mbigili), Mkoani Morogoro kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *