VIKUNDI VYA BUSTANI KUTOA FURSA ZAIDI ZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Vikundi vya Kilimo cha Umwagiliaji ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini vimejipanga kutoa elimu itakayohamasisha vijana  na akina Mama  kuchangamkia fursa za kilimo cha umwagiliaji  hasa kwa jamii zinazoishi karibu na vyanzo vya maji mengi yanayoweza kutumika kwenye umwagiliaji.

Hayo yamesemwa na  Gudluck Wambwe ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET cha Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi.

Ad
KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Wanakikundi cha NO SWEAT NO SWEET wa Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi,wakiwa kwenye shamba la matikiti maji.

Kikundi hicho cha Kijijini Bugunda, kwa kipindi kirefu kimekuwa kikijishughulisha na Kilimo cha Bustani za Mbogamboga na Matunda.

Ndugu Gudluck Wambwe amesema kuwa, wamekuwa wakipata maarifa ya Kilimo cha Umwagiliaji kutoka kwa Mtaalamu wa Kilimo wa Kata yao.

Ameongezea kuwa “Kupitia Kilimo cha Umwagiliaji tayari wamekwishanufaika na faida za Kilimo hicho ni nyingi zikiwemo, kuwa na uwezo wa kifedha wa kugharimia mahitaji ya shule ya watoto wao, na kujipatia mahitaji mbalimbali ya kifamilia.”

KIKUNDI CHA NO SEAT NO SWEET
Wanakikundi cha NO SWEAT NO SWEET wa Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi,wakiwa kwenye shamba la matikiti maji.

Aidha, Kiongozi huyo amesema kuwa, malengo yao ya sasa ni kuielimisha jamii kuhusu Kilimo cha Umwagiliaji tofauti na ilivyozoeleka hapo awali kujikita kwenye Kilimo cha Asili (msimu wa mvua) peke yake.

Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata, Ndugu Gustav Tesha alieleza kuwa, anaendelea kuwapa elimu wakazi wa Kata za Bulinga na Bwasi juu ya Kilimo cha Umwagiliaji na anakiri kwamba jamii imekubali kubadilika na kuwa na mtazamo mpya wenye kuleta matokeo chanya kwa kushiriki katika Kilimo cha Umwagiliaji.

NO SWEAT NO
Wanakikundi cha NO SWEAT NO SWEET wa Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi,wakiwa kwenye shamba lao wakiendelea na kazi ambapo wanafanya kilimo cha umwagiliaji.

Ikumbukwe kuwa, Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET ni moja kati ya Vikundi 15 vilivyofadhiliwa Pampu, Mipira ya umwagiliaji na Mbegu kutoka kwenye Mgao wa fedha za mfuko wa Jimbo awamu ya kwanza.

Wanakikundi na Washiriki wa Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET wanamshukuru Mbunge wao Prof. Muhongo kwa juhudi zake za kuipa kipaumbele Sekta ya Kilimo cha Kisasa na chenye Manufaa ili kuinua Uchumi wa Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na wanasema kwao Kilimo ni Ajira.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *