Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Seleiman.

PROF.KABUDI AKUTANA NA WAZIRI WA KATIBA WA SMZ

  • Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Seleiman.
  • Prof. Kabudi yuko Zanzibar kwa ziara ya siku mbili na katika mazugumzo yao wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya Wizara zao katika mambo yote yanahohusu na yasiyohusu Muungano.
Prof. Kabudi Waziri wa Sharia na Katiba
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi wa upande wa kulia akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Seleiman.
  • Mawaziri hao wamesisitiza umuhimu wa Wizara zao kuendeleza ushirikiano katika maeneo ya utungaji wa Sheria, kushirikiana kwenye mafunzo ya Mahakimu, waendesha mashtaka na waandishi wa Sheria.
  • Kwa pamoja wamekubaliana kukaa na kubainisha maeneo ambayo yanahitaji kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika.
Waziri wa Sheria na Katiba
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Seleiman.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga zaidi ya shilingi bilioni 250 katika mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi katika Halmashauri zote 184 nchini

Taarifa hii imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *